Katibu Mkuu Dkt.Servacius
Likwelile akiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Kanda ya
Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu katika Mkutano uliofanyika katika ukumb wa
Ecobank Jijini Kigali Rwanda.
Mh.Waziri wa Fedha Saada
Mkuya Salum akijadiliana jambo na mmoja wa washiriki wa Mkutano wa 49 wa Benki
ya Maendeleo ya Afrika unafanyika Kigali Rwanda. Pembeni ni mwa Waziri ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na msaidizi wa Waziri
Bw.Thomas Mabeba.
Waziri wa Fedha Mh.Saada
Mkuya Salum akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkuatno mkuu wa mwaka wa benki ya
maendeleo ya Afrika uliofanyika Kigali Nchini Rwanda.
Mkutano Mkuu wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika umemalizika
Jijini Kigali,Rwanda kwa Viongozi wa Benki kuahidi kujenga Afrika ambayo ni
itakuwa na Umoja,mshikamano na yenye miundombinu ya uhakika.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika,Dkt. Donald Kaberuka amesema Benki
itasaidia utekelezaji wa mipango bora ambayo itatokana na majadiliano
yatakayofikiwa kwenye vikao nchi wananchama. Miongoni mwa vipaumbele vya benki
kwa kipindi cha miaka kumi ijayo ni kujenga mazingira ya kuwa na uchumi imara
na endelevu,usimamizi wa maliasili za bara la Afrika na ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha zaidi wanawake na vijana katika ukuaji wa uchumi wa bara la
Afrika.
Katika kuhakikisha maendeleo ya Bara la Afrika yanafikiwa kupitia Benki
ya Maendeleo ya Afrika kwa kipindi cha miaka 50 ijayo ni pamoka na kusimamia
utekelezaji wa mpango wa ‘Afrika 50’ ambao utapelekea kuongeza ufadhili wa
kiasi cha Dola bilioni 100 ambazo zinahitajika katika kuimarisha miundombinu ya
Bara la Afrika.
Awali katika mkutano uliofanyika kati ya Mkurugenzi wa AfDB kanda ya
Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu na ujumbe wa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile aliishukuru benki kwa jitihada zake za
kuhakikisha Tanzania inatekeleza kwa ufanisi miradi yote inayofadhiliwa na
Benki hiyo. ‘Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika ambayo
inanufaika na fedha kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika,kwa sasa tuna zaidi ya
miradi 31 ambayo inatekelezwa na AfDB’ alisema Dkt.Likwilile.
Mwishoni mwa Mkutano wa Magavana wa Benki,Pia walipitisha kuanzishwa kwa
‘Africa Growing Together Fund (AGTF)’,na kiasi cha dola bilioni 2 zitatolewa na
china ili kuwezesha AfDB kukabiliana na kuongezeka kwa mahitaji ya kikanda kwa
nchi wanachama wa benki na wateja wa sekta binafsi.
Mkutano ujao wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika utafanyika Jijini
Abidjan,nchini Ivory coast ambayo pia itakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka
50 ya benki ya maendeleo ya Afrika yatakayoadhimishwa Novemba,2015.
0 Comments