6/recent/ticker-posts

Kikosi cha PBZ chatoa kipigo kwa timu ya ZAWA.

Kikosi cha timu ya Benki ya Watu wa Zanzibar kilichotowa kipigo kwa Timu ya Mamlaka ya Maji Zanzibaer (ZAWA) katika mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan, Mchezo wa kumuaga Bosi wao Ndg. Ame Haji Makame ambae amestaaf kuitumikia PBZ kwa miaka zaidi ya 40.Ushindi huo ni zawadi kwa Bosi wao huo, na moja ya mazoezi ya kujiandaa na michezo ya mahoteli inayotarajiwa kuazi hivi karibu mchezohuo ukiwa ni moja ya mandalizi ya michuano hiyo.  
Mziki wa kikosi cha PBZ kikipasha misuli motokabla ya kuaza kwa mchezo wao na ZAWA, uliofanyika uwanja wa Amaan na kuibuka na ushindi wa bao moja. 
                                                 Pasha pasha ushindi ndio kazi yetu
                   Mashine ya timu ya PBZ ikipasha moto misuli kabla ya mchezo huo na timu ya ZAWA.
Wachezaji wa timu ya PBZ wakiwa na tabasamu kabla ya kuaza kwamchezo wao wa kujipima nguvu na timu ya ZAWA, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan. 
Kiungomchezeshaji wa Kikosi cha PBZ akipasha misuli kabla ya mchezo kuaza uwanja wa Amaan.
Mchezaji wa timu ya PBZ akimpita beki wa timu ya ZAWA, katika mchezo wa kirafiki na kwa maandalizi ya timu ya PBZ na michezo ya mahoteli.  

                                Mshambuliaji wa timu ya PBZ akimpita beki wa timu ya ZAWA.
Mchezaji wa timu ya PBZ akimpita beki wa timu ya ZAWA katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan, timu ya PBZ imeshinda mchezo huo kwa balomlililofungwa na mchezaji Rashid Mohammed katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza cha mchezo huo.hadi mwisho PBZ imetoka kifua mbele kwa bao  1---0.



Ula umepita wewe mpira umebaki kwangu ndivyo beki wa timu ya ZAWA akinena baada yamzuiya mshambuliaji wa timu ya PBZ.
Viongozi wa benchi la timu ya ZAWA wakiwa na mshangao baada timu yao kulala kwa bao 1--0 dhidi ya timu ya PBZ. 
Mshambuliaji wa timu ya PBZ akimpita beki wa timu ya ZAWA katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan. timu ya PBZ imeshinda 1--0.
Mchezaji wa PBZ akijaribu kuzuiwa mpira mbele ya beki wa ZAWA, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan ukiwa ni maalum kwa ajili ya kumuaga Bosi wao Ndg Ame Haji Makame. wameweza kumpa zawadi ya ushindi wa bao 1--0. 
                              Mchezaji wa timu ya PBZ akimpita beki wa timu ya ZAWA.

Wachezaji wa timu ya ZAWA wakiwa mapumziko wakipata mawaidha jinsi ya kutoka na ushindi dhidi ya wapizani wao PBZ. 
Kiongozi wa timu ya PBZ akitowa maelekezo kwa wachezaji wa timu yake wakiwa mbele kwa bao moja dhidi ya ZAWA, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.
                         Beki wa timu yaZAWA akimzuiya mshambuliaji wa timu ya PBZ
Benchi Viongozi la timu ya PBZ wakifuatilia mchezo wao huo maalum dhidi ya timu ya ZAWA uliofanyika katika kiwanja cha Amaan Zanzibar na kuibuka na ushindi mdogo wa bao 1--0.

Post a Comment

0 Comments