Na Mwandishi Wetu.
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itahakikisha kuwa inazingatia mambo
matatu makuu katika ukuaji wa uchumi wa Zanzibar .
Mambo hayo ni pamoja na kutilia mkazo ukusanyaji na udhibiti
bora wa mapato ili kuhakikisha malengo yaliokusudiwa yanaweza kufikiwa kwa
wakati na kwa kiwango kilichokusudiwa.
Waziri wa fedha Mhe. Omar Yussuf Mzee, aliyasema hayo katika
kikao cha baraza akijibu hoja za Wajumbe mbalimbali walizozitoa wakati
wakichangia bajeti kuu ya Serekali ya
Mapinduzi Zanzibar ya mwaka wa fedha 2014/2015.
Waziri huyo alitaja jambo jingine ambalo Serekali inakusudia
kulizingatia katika ukuaji wa Uchumi wa Zanzibar
ni uibukaji wa vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaweza kuleta tija na manufaa
katika ukuwaji wa uchumi.
Sambamba na hilo lakini
Waziri huyo alisema Serekali itasimamia utulivu na kutilia mkazo suala la
kuwepo kwa amani Zanzibar ,
hasaikizingatiwa kwamba suala la amani ndio nyezo muhimu katika kuimarisha
hatua za kimaendeleo nchini.
Eneo jengine ambalo litasimamiwa ni kubaini wanaokwenda kodi
na kuhakikisha wanafuata utaratibu wan a sheria za ulipaji kodi. Alisema.
Kuhusu Bajeti alisema Serekali imekuwa ikipata msaada wa
asilimia 4.5 wa bajeti kutoka kwa wafadhili kila mwaka.
Waziri Omar alisema serekali kwa kuona umuhimu wa
wafanyakazi hususani wataalamu, imeimarisha viwango vya mishahara kwa lengo la
kuhakikisha wataalamu hao wanaendelea kutumikia nchini hasa katika sekta ya
Afya na Elimu.
Pamoja na hayo alisema hatua nyegine ambayo serekali
imekusudia ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji kuazisha viwanda nchini kwa
lengo la kupanua zaidi masuala ya kibiashara ambayo yataweza kutoa fursa za
ajira kwa vijana.
Akizungumzia suala la Mikopo ya nchi ambapo baadhi ya
wajumbe walitaka ufafanuzi kuhusu madeni ya nchi na athari zake kiuchumi,
alisema kukopa sio kuteremka kwa uchumi wa nchi kwani hata nchi zilizoendelea
zimekuwa zikikopa, ila suala la msingi ni kuzingatia mikopo hiyoitumike kwa
masuala ya kimaendeleo ambayo yatakuwa yanainua uchumi wa nchi.
Akijibu hoja kuhusu suala la utegemezi alisema kwamba
linaweza kuondoa uwepo wananchi wataendeleaza umoja na kuondokana na suala
lakubaguana wenyewe kwa wenyewe.
Alisema kodi zinazokusanywa zinawanufaisha wananchi wote
kupitia sekta mbalimbali ambazo kodi hizo hutumika katika masuala ya
kimaendeleo.
Wakati akijibu hoja kuhusu namna ya kuisaidia sekta ya
huduma, waziri alisema kwamba serekali inakusudia kuangalia upya namna ya
kuipanua sekta hiyo ili iweze kuleta tija zaidi kwa uchumi wa nchi. .
0 Comments