6/recent/ticker-posts

Ujuwe kwa Ufupi Mji wa Kiruna Sweden

Mji wa Kiruna uliopo nchini Sweden unapatikana kilomita 145 kaskazini ya duara liitwalo "Artic" (artic circle). Kiuchumi mji huu unategemea sana madini ya chupa cha pua. Upo mgodi wa chuma cha pua ambao ni mkubwa sana na ni wa sasa kabisa kuliko mgodi mwengine wowote duniani. Ndani ya mgodi ni kama ndani ya nyumba ya kisasa. Umaarufu mwengine wa mji huu ni kuwepo kwa kituo cha anga (space center) kinachomilikiwa na nchi za Jumuiya  ya Ulaya. kwa upande wa utalii Kiruna inajivunia kuwepo kwa hoteli ya barafu (icehotel) ambayo hujengwa wakati wa majira ya baridi. Hoteli hii huingiza fedha nyingi sana kwani wanaolala  ni watalii wa daraja la juu. Maajabu mengine ya mji huu yanaonekana kipindi hiki ambacho ujumbe wa wadi za Makunduchi upo. Hivi sasa hakuna usiku hapa kwa maana ya usiku wa nyumbani wakuwa na giza kwani muangaza wa jua upo wakati wote saa 24. Hali hii itaendelea hadi mwanzoni mwa mwezi wa Agosti. Saa zote saa 24 ni kweupe umekucha. Aidha kipindi cha kuwa na giza saa 24 pia kipo katika mji huu kwenye miezi ya Disemba hadi Januari. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mkubwa!

Aina moja wapo ya mfano wa vyombo vinavyorushwa angani na kitua cha anga cha Kiruna.

Post a Comment

0 Comments