Na Mwandishi Wetu
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar imesema hakuna shria yoyote
itakayoweza kuchukuliwa dhidi ya Mjumbe wa baraza la Wawakilishi kwa kuzungumza
na kujadili mambo mbalimbali wakiwa ndani ya vikao vya baraza na Bunge.
Serekali imesema kila baraza au Mabunge yoyote duniani
yanalindwa na kanuni zake hivyo mjumbe yoyote wa baraza anaweza kuzungumza
ndani ya baraza maelezo yake yote aliyoyasema na hatafunguliwa mashtaka ya
madai au jinai.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, alipokuwa
akijibu suali la Mwakilishi wa jimbo la Wawi Pemba Mhe. Saleh Nassor Juma,
alietaka kujua Sheria ya Zanzibar zinasemaje kwa Waheshimiwa wanaokwenda
kinyume na kiapo walichoapa juu ya kuiteteaKatiba ya Zanzibar .
Waziri Aboud alisema sheria ya Baraza la Wawakilishi (kinga
maalum na fursa) namba 4 ya mwaka 2007 kifungu cha tatu na kifungu cha nne
kimeweka kinga kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa na uhuru wa kuzungumza
na kujadili wakiwa ndani ya vikao vya baraza na uhuru huo hautohojiwa na
mahakama yoyote au sehemu yoyote nje ya Baraza.
Awali katika suala la msingi la Mwakilishi huyo alitaka
kujua Sheria za Zanzibar
zinasemeja kwa Waheshimiwa wanaokwenda kinyume na kiapo walichoapa.
Mwakilishi huyo alifahamisha kuwa katika kutekeleza kazi zao
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walikula kiapo cha kulinda, kuituza na
kuitetea Katiba ya Zanzibar lakini kuna baadhi yao wanakwenda kinyume na
kiapo hicho.
Alisema kuna baadhi ya wajumbe wa baraza ambao pia ni
wajumbe wa bungev la katiba wamethubutu kuikebehi Katiba ya Zanzibar na
kuilinganisha na katiba ya timu za mpira
sambamba na kulinganisha na bendera za
Simba na Yanga pamoja na ile ya Uamsho.
Waziri Aboud akijibu suali la nyongeza la mwakilishi huyo,
alisema ni vyema ikatumika lugha ya staha kwa viongozi pamoja na nchi ili kulinda heshima ya baraza
pamoja na viongozi wake.
0 Comments