Na Mwandishi Wetu.
Kutokuwepo kwa sheria ya
kuwabana waharibifu wa mazingira ya
misitu kunasababisha uharibifu kuongezeka nchini hapa.
Hayo yelielezwa na Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Uhifadhi Mazingira wa Kikundi cha Kumsa, Ndg Voti Mtumwa Mkadam,
alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii huko kiwengwa wilaya ya
Kaskazini B Unguja.
Alisema hali hiyo ya
uharibifu wa mazingira unasababisha ongezeko kubwa la uharibifu mazingira kwa
kasi kubwa na kusababisha nchi kugeuka na kuwa jangwa.
Alifahamisha kuna baadhi ya
vyombo vya sheria havitendi haki kwa vile wanakuwa wanawaachilia wananchi
wanaoharibu misitu bila ya kuwapatia adhabu yoyote, jambo amnalo linatejesha
nyuma juhudi za kuzuia uharibifu huo.
Alisema licha ya kuwepo kwa utoaji
wa elimu ya utunzaji wa mazingira, lakini bado kuna wananchi kila kukicha
wanaendelea kukata misitu hali ambayo inasababisha maporomoko ya ardhi pamoja
na kupotea kwa rasilimali hizo.
Kila mmoja ana jukumun la
kutunza mazingira na kuhakikisha kuwa ni mlizi wa nafasi yake na mlizi wa
mweziwe yoyote atakayeonekana anafanya kitendo hicho cha uharibifu wa
mazigira,hatua kali zichukuliwe juu yake na hakuna msamaha,alisema Mwenyekiti
huyu kwa uchungu.
Mwenyekiti huyo alisema kwa
sasa athari zimejitokeza kwa wingi ikiwa ni pamoja na bahari kuja juu kwa kasi
sasa pamoja na ongezeko kubwa la joto,hivyo ni vyema kuwa tayari kukabiliana na
athari hizo.
Aidha, alisema katika
kuhakikisha uharibifu wa misitu unadhibitiwa ni vyema kuwa na ushirikiano
madhubuti baina ya wananchi na jeshi la Polisi ilikuona kwamba uharibifu wa
misitu unaondoka hapa nchini kwetu.
0 Comments