Na Himid Choko BLW.
DAR ES SALAAM July 14, 2014
Kamati ya mashauriano ya bunge Maalum la
Katiba inatarajiwa kukutana kutathmini kazi zilizofikiwa za utungaji wa katiba mpya ya Tanzania.
Kamati
hiyo inatarajiwa kukutana kwa siku mbili kuanzia tarehe 24 mwezi huu katika ofisi ndogo
za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Daresalaam.
Taarifa
iliyotolewa na katibu wa bunge maalum la
katiba Yahya Khamis Hamad imeeleza kuwa kamati hiyo inawajumuisha wajumbe
thelathini walioteliwa na Mwenyekti wa bunge hilo Mh Samwel Sita kwa kushirikiana na Makamu
wake Mh Samia Suluhu Hassan.
Uteuzi
wa wajumbe wa kamati hiyo ya mashauriano ya bunge hilo ni kwa mujibu wa masharti
ya kanuni ya 54(4) na (5) ya kanuni za Bunge
Maalum za mwaka 2014.
Taarifa
hiyo imewaomba wajumbe walioteuliwa kuhuduhria kikao hicho kwa lengo la
kufanikisha kazi waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
niaba ya Watanzania.
0 Comments