Na Shemsia
Khamis, Pemba
OFISA Elimu
na Mafunzo ya Amali wilaya ya Wete, Khamis Said Hamad, amesema, vitendo vya
ukatili dhidi ya wanawake na watoto, havipaswi kunyamaziwa
Alisema hayo
wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya Kinyikani wilaya ya Wete, katika
mkutano maalumu wa kuhamasisha jamii namna ya kuyaripoti vitendo hivyo
uliondaliwa na wananchi hao.
Alisema
kumeundwa taasisi mbali mbali zinazoendesha mapambano hayo, lakini bado jamii
haina mwamko wa kutoa ushahidi pale wahusika wanapofikishwa kwenye vyombo vya
sheria.
Alisema vitendo
vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimekithiri katika jamii hivyo kina mtu
ana wajibu wa kukabiliana navyo.
Kwa upande
wake, Mratibu wa wanawake na watoto shehia ya Kinyikani, Muwa Siad Khamis,
alisema katika shehia yake kuna baadhi ya watu wanavifumbia macho vitendo hivyo
na kushindwa kutoa ushirikiano.
Sheha wa
shehia ya Kinyikani,Mussa Rashid Said,alisema licha ya wanaharakati kuwa mstari
wa mbele kupinga udhalilishaji, bado jamii yenyewe haijataka kubadilika.
Akizungumza
katika mkutano kama huo uliofanyika shehia ya Kiungoni,mwanaharakati kutoka
Wizara ya Wanawake na Watoto, Dina Juma Makota, alisema watoto wana haki yao
Mikutano
hiyo ilifanyika chini ya ufadhili wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania
(TAMWA).
0 Comments