Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua, Dk. Charles Msonde, kuwa Katibu Mtendaji wa
Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania
(NECTA).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam na
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema uteuzi huo ulianza Jumatano,
Agosti 13, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, Dk. Msonde alikuwa
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo .
Msonde anachukua nafasi iliyoachwa wazi
na Dk. Joyce Ndalichako, ambaye amerudi kuendelea na kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya
kumaliza likizo yake ya kujinoa.
0 Comments