JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 31 Ogasti, 2014
| Taarifa kwa umma: Upepo mkali unaoambatana na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika maeneo yote ya ukanda wa Pwani. Taarifa Na. | 201408-02 |
|
Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki |
Saa 6:00 Mchana |
| Daraja la Taarifa: | Tahadhari |
|
Kuanzia: Tarehe |
01 Septemba, 2014 |
|
Mpaka: Tarehe |
02 Septemba, 2014 |
| Aina ya Tukio Linalotarajiwa | Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 inatarajiwa katika ukanda wote wa Pwani. |
| Kiwango cha uhakika: | Juu: (70%) |
| Maeneo yatakayoathirika | Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. |
| Maelezo: | Hali hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika maeneo ya kusini mwa Afrika hivyo kusababisha upepo mkali wa Kusi, mashariki mwa Pwani ya Tanzania. |
| Angalizo: | Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari. |
| Maelezo ya Ziada | Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi. |
0 Comments