Na
Juma Khamis
MAMLAKA
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ofisi ya Zanzibar, imeanza zoezi la utoaji wa
vitambulisho vya taifa kwa wananchi wa wilaya ya kaskazini ‘A’ Unguja.
Akizungumza
na wanahabari jana, Mkurugenzi wa NIDA ofisi ya Zanziba, Vuai Mussa Suleiman,
alisema vitambulisho hivyo vinatolewa kwa utaratibu maalum uliowekwa.
Shehia
ambazo vitambulisho hivyo vitaanza kutolewa ni Bandamaji,Kinyasini,Kandwi,Pwani
Mchangani,Kisongoni,Matemwe, Kivunge,Mkwajuni, Kidombo,Kidoti , Moga, Gamba na
Muwange.
Alisema
vitambulisho vitatolewa kwa siku tano kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo
wananchi ambao majina yao yamo kwenye orodha watatakiwa kwenda kwenye vituo
vyao walivyojiandikisha.
Kwa
upande wa utoaji wa vitambulisho kwa maidara na taasisi za serikali kisiwani
Pemba alisema limeanza jana.
Aliwataka
wananchi wanapokwenda kuchukua vitambulisho vyao wachukue stakabadhi walizopewa
wakati wa kujiandikisha na kama zimepotea wachukue vitambulisho vyengine
walivyovitumia wakati wa kujiandikisha.
Aidha
alisema NIDA tayari imeshafungua ofisi
katika wilaya zote za Zanzibar isipokuwa wilaya za kaskazini B Unguja na kusini
ambazo hazijakamilisha masuala ya kiutawala.
Alisema
lengo la kufungua ofisi hizo ni kuwahudumia wananchi ambao hawakuwahi
kusajiliwa wakati wa zoezi la awali.
Hata
hivyo, alisema NIDA inakabiliwa na changamoto mbali mbvali ikiwemo wananchi
kutotumia fursa ya kupelekewa vitambulisho vyao katika maeneo wanayoishi badala
yake wanalazimika kuvifuata ofisi za wilaya.
Pia alisema baadhi ya
wananchi wameshapoteza vitambulisho vyao kutokana na utunzaji mbaya hivyo
kulazimika kwenda mamlaka kuomba
chengine wakati wenzao hawajapatiwa hata mara
0 Comments