Na Mwanajuma Abdi, Dar es
Salaam
SERIKALI ya Finland imekabidhi hundi ya
shilingi milioni 150, kwa washindi 10 wa tunzo ya ubunifu wa mfumo wa habari na
mawasiliano yanayorahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Hafla hiyo imefanyika jana
katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam,
ambapo Balozi wa Finland nchini Tanzania,
Sinikka Antila, alikabidhi hundi hizo mbele ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Patrick Makungu,
aliyemuakilisha Waziri wa Wizara hiyo,
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa.
Alisema fedha walizokabidhiwa
vijana 10 kutoka kampuni mbali mbali za ubunifu waliotengeza ‘software’ kupitia
mawasiliano ya kompyuta na smart phone, ambazo zinarahisisha upatikanaji wa
bidhaa mbali mbali kupitia TEHAMA.
Alisema serikali yake kwa
kushirikiana na Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania, wameanzisha mfuko wa
kuwasaidia wabunifu ikiwa ni mradi wa kukuza maendeleo nchini hususani kwa vijana
wajasiriamali.
Alisema malengo hayo yanakwenda
sambamba na dira ya maendeleo ya Tanzania ya ukuaji wa kati wa uchumi ifikapo
mwaka 2025, katika kuimarisha uzalishaji
wa bidhaa katika sekta mbali mbali, hivyo kuwepo kwa wabunifu hao kutatoa fursa
kwa wenzao kuajiri na kukabiliana na masoko katika ulimwengu wa utandawazi.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Patrick Makungu kwa niaba ya waziri
wake, alisema ubunifu unasaidia kuzalisha ajira kwa vijana, ambapo fedha walizokabidhiwa
zitasaidia kuzalisha ajira za heshima kwa wenzao.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Hassan Mshinda, alisema ubunifu huo utaisaidia
jamii kununua bidhaa za biashara nje na ndani ya nchi kupitia sekta ya habari
na mwasiliano (TEHAMA).
Nao washindi hao, walisema walijishindia
fedha hizo baada ya kutengeneza software katika kompyuta na kuingiza taarifa za
bidhaa kupitia teknolojia hiyo ambapo mtu aliyeko eneo lolote anaweza kujua
habari ya bidhaa hiyo.
0 Comments