6/recent/ticker-posts

Polisi wajipanga kuwashughulikiwa wauza ‘unga’

Na Masanja Mabula, Pemba
KAMISHNA wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, amekiri baadhi ya maeneo ya visiwa vya Zanzibar yanatumika kuingiza dawa za kulevya.

Alisema mwarubaini pekee  wa kukabiliana na tatizo hilo ni jamii  kuwafichua waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa hizo.

Alisema jamii inawatambua waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya katika maeneo yao na kuwataka kuondoa muhali kwa kutoa taarifa polisi ili wachukuliwe hatua.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kisiwani Pemba, alisema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa kupitia falsafa ya polisi jamii, bado uingizaji, usambazaji na utumiaji wa madawa hizo unaendelea.


Aidha alikiri baadhi ya maeneo katika kisiwa cha Pemba kuwa kitovu ya uingiaji wa dawa za kulevya na kuongeza kwamba wamejipanga kuyadhibiti maeneo yao hasa yenye bandari bubu kwa kuimarisha ulinzi na doria.

Aliwataka wananchi kuacha fikira hasi ya kwamba biashara ya dawa za kulevya ni hahali kwa kuwa inawapatia fedha.

Alisema vijana wengi ambao wamejiingiza katika wimbi la utumiaji wa dawa za kulevya wameishia jela kutokana na kushiriki uhalifu.


Maeneo ambayo yanaonekana kukithiri vitendo vya uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya katika mkoa wa kaskazini Pemba ni Mtambwe ambapo kuna bandari bubu nyingi na sheha ya Bopwe.

Post a Comment

3 Comments

  1. ''mwarubaini pekee wa kukabiliana na tatizo hilo ni jamii kuwafichua waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa hizo'' Hivi commissioner tuwafichuwe vipi anavyotaka wewe hebu tufafanulie? maneno yako unamaanisha kama hilijambo ni la jamii pekeyao na huku kijiona nyinyi sio party ya jamii. Wananchi wana-report ila jeshi lenu limepoteza maadili kwakweli. Hii imefikia mpaka wananchi kutoliheshimu kwa ukosefu wa nidhamu na tamaa ya watendaji wa jeshi la police. Wewe binafsi hakika wajuwa kuwa kutokana na hali halisi ya tamaa za watendaji wenu wamekuwa so waaminifu na nyinyi ndio chanzo cha kuenea janga hili la drugs. Jiulizemiaka ya 80 kweli ndio jeshi hili la leo? Miaka ya nyuma police wakiheshimiwa nawanachi kwakuwa walikuwa waadilifu na wenye nidhamu ya pekee kwa jamii. Mimi ningepata dakika moja kumshauri Rais basi lakwanza ni hili la drugs. Ningemwambia Mh Rais immediately awakabidhi Jeshi la wananchi (JWTZ) vita hivi vya madawa ya kulevya. Hii ninamini kuwa jeshi pekee ambalo lina nidhamu na hawapo corrupted ni jeshi la JWTZ. Ningemshauri akodi administration yao, na kwa uhakika within six moth nchi ingekuwa safi. Ila kwa nyinyi police NO mmeshindwa vita hivi na sikwakuwa ni jambo la siri lah, rushwa ndio imepoteza heshima yenu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. aisee umenifurahisha vibaya mno kwani umesema kweli tupu mungu akubarik.

      Delete
  2. Nakubaliana na mchangiaji wa kwanza kwamba hili jambo wapewe JWTZ walishughulikie. Commissioner wewe kweli huwajuu wanaoingiza madawa la kulevya au unataka kujifurahisha tu? Mimi siamini kama nyinyi vigogo wa jeshi la polisi hamuwajui waingizaji kwa sababu nyinyi ndio munaocheza nao michezo ili mupewe chenu (Percentage %). Nimesema hayo kwa sababu dalili zote zinaonesha hivyo na kwa mfano mdogo tu katika mahojiano aliewekwa katika mtandao huu kama week mbili nyuma kama sijakosea, baina ya aliekuwa anatumia madawa kulevya na inaonesha wazi munajua kila kitu isipokuwa mumeendekeza tamaa badala ya kuwajibika. Nyinyi ndio chanzo cha kuua nguvu ya jamii kwa tamaa zenu.
    Nakushauri Commissioner kama kweli unataka kuiokoa jamii kwa hili jangwa basi fanya haya:

    1. Lijenge jeshi lako liwe linafanya kazi kwa uadilifu kwa kufata sheria za nchi na sio kufata hisia zenu mana ndizo zinazokusabibishieni mule rushwa na kuwajibika kisiasa badala ya kitaaluma yenu.

    2. Shughulikia mzizi wa hili tatizo kwa kuwashughulikia vigogo wanaoleta haya madawa bila ya kujali cheo chake au umaarufu wake.

    Hayo yote munaweza mukiamua kubadilika.
    shukrani...Kazi njema

    ReplyDelete