Jukwaa la Sauti za Busara likiwa hewani kutowa burudani kwa Wageni na Wananchi wa Zanzibar wakati wa ufunguzi huo. uliofanyika kwa matembezi ya fensi yalioazia viwanja vya tumbaku hadi viwanja vya Ngomekongwe.
Kikosi cha Reki kikiwa katika matembezi ya Fensi ya Tamasha la Busara wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo uliofanyika leo 12-2-2015, wakipita katika mitaa ya michezani wakielekea viwanja vya ngombekongwe Zanzibar.
Wasanii wa ngongoti wakishiriki katika maandamano hayo ya ufunguzi wa Sauti za Busara Zanzibar wakipita katika mitaa ya michezani Zanzibar.
Kikundi cha Wasanii Sengembuke na Halikuniki wakiwafa vitu vyao wakati wa maandamano hayo. yakielekea viwanja vya ngomekongwe.
Vijana wa Kikundi cha Smart Zanzibar wakiwa bango lao lenye Ujumbe" VIJANA NDIO NGUZO YETU" wakiwa katika maandamano hayo
Wanafunzi wa Skuli ya SOS wakishiriki katika maandamano hayo wakiwa na Walimu wao.
Nao Vijana wa Jumuiya ya Michezo ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar wakishiriki katika maandamano hayo ya Fensi ya Ufunguzi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa Zanzibar wakiwa katika ngoma ya Mwanandege wakipita katika mitaa ya Mji Mkongwe Zenj wakielekea katika viwanja vya Ngome Kongwe
Vijana wa Kikundi cha Smart kutoka Zanzibar wakionesha.
Msanii kutoka Afrika ya Kusini Ihhashi Elimhlophe, akishirika kastika masandamano ya fensi ya ufunguzi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar wakati wa ufunguzi.
Wasanii wa Kimasai wakionesha Utamaduni wa Ngoma yao wakiwa katika maandamano ya Fensi ya Ufunguzi wa Tamasha la Sauti za Busara.
Wageni mbalimbali waliotembelea Zanzibar wakipata picha ya kumbukumbu za ufunguzi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar wakati wasanii wakiwa katika maandamano ya Fensi yakipita katika mitaa ya Mji Mkongwe Zenj.
Wasanii wakiwa katika viwanja vya Ngomekongwe wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo
Wasanii wa kutoka Visiwa vya Mayotte wakitowa burudani ya maulid ya homu katika viwanja vya forodhani
1 Comments
Zanzibar carnival.
ReplyDelete