6/recent/ticker-posts

‘Mahakama inachelewesha kesi za uchaguzi’

Na Haji Nassor, Pemba
MAJAJI na Mahakimu nchini, wameshauriwa kuzitolea maamuzi ya haraka kesi zinazohusiana na uchaguzi,badala ya kuziweka hadi miaka mitatu kwani kufanya hivyo kunaondoa maana kwa wananachi au vyama kulalamika uchaguzi mahakamani.
Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,Mwanajuma Majid Abdalla, alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya sheria Zanzibar yaliyofanyika uwanja wa tenis mjini Chake Chake Pemba.
Alisema ili wananchi na vyama vione umuhimu wa kupeleka kesi zao mahakamani pale wanapoona hawakutendewa haki kwenye chaguzi, basi ni vyema uamuzi ukatolewa kwa wakati muafaka.
Alisema kesi kama za uchaguzi hazifai kuendeshwa pole pole hadi kufikia kuvuka miaka mitatu, na kufanya hivyo ni kupoteza maana.
“Sio busara hata kidogo kuona kesi za uchaguzi zinakaa muda mrefu mahakamani, kwani kufanya hivyo hakuleti maana hata kidogo kwa vyama au wananchi kulalamikia uchaguzi,”alifanaua.

Katika hatua nyengine, Mkuu huyo wa Mkoa  aliwataka Mahakimu na Majaji kuendelea kutoa haki kwa wanaostahili.
Kwa upande wake wakili wa kujitegemea,Yussuf Mohamed, wakati akisoma risala kwa niaba ya wanasheria wa kujitegemea, alisema bado baadhi ya Mahakimu na Majaji wamekuwa wakizizorotesha kesi zinazohusiana na uchaguzi.
Alitoa mfano kwamba tokea kumalizika kwa uchguzi mdogo wa jimbo la Bububu Unguja mwaka 2012 hadi leo kesi hiyo imeshindwa kutolewa uamuzi.
Aidha alisikitishwa na kitendo cha baadhi ya Majaji, Mahakimu na Waendesha Mashitaka, kuingilia kazi zao na kuwapa wakati mgumu wanapokua mahakamani.
Hata hivyo, alisema kutokuwepo kwa Majaji wakaazi kisiwani Pemba kati ya wale sita waliopo kisiwa cha Unguja, husababisha mrundikano wa kesi kwenye mahakama kuu.

Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, Mkusa Issac Sepetu, alisema changamoto ya uchakavu wa majengo ya mahakama tayari imeanza kutatuliwa, kwa kufanyiwa matengenezo makubwa Unguja na Pemba.

Post a Comment

0 Comments