Na Kija Elias, Rombo
WANANCHI wa kijiji cha
Aleni wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, wamevamia jengo la ofisi ya idara ya kilimo
na umwagiliaji na kisha kulichoma moto kupinga kuondolewa kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho kwenye jengo
la Chama cha Mapinduzi na kuhamia kwenye jengo la idara hiyo.
Kuchomwa kwa jengo hilo
kunafuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, aliyoitoa hivi karibuni ya
kupiga marufuku viongozi wa serikali za mitaa wanaoishi kwenye nyumba
zinazomilikiwa na CCM.
Akizungumza na Zanzibar
Leo, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya
Rombo, Elinas Pallangyo, alisema tukio la kuchomwa moto kwa jengo hilo limetokea
baada ya Mwenyekiti wa kijiji hicho kuagizwa kuondoka kwenye jengo la CCM na kuhamia
kwenye jengo la idara ya kilimo.
Alisema tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia FebruarI 9 mwaka huu ambapo wananchi hao wanadai
majengo ya CCM ni mali ya wananchi kwani yalijengwa kwa michago ya wananchi na
si ya chama.
Alifafanua kuwa ofisi
hiyo imeteketea pamoja na mali zote ambapo mpaka sasa thamani halisi
haijajulikana na jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahusika.
0 Comments