6/recent/ticker-posts

Wafanyabiashara jumba la reli waingia mitini

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema haitobadilisha uamuzi wake wa kulifanyia ukarabati jumba la treni liliopo eneo la biashara Darajani ambalo lipo hatarini kuporomoka.

Waziri wa Ardhi, Makazi Maji na Nishati, Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban, aliyasema hayo katika ukumbi wa Mamlaka ya Mji Mokongwe kabla ya kuvunja kikao, kutona na wafanyabiashara katika jumba kuingia mitini.

Alisema uamuzi wa serikali wa kuwahamisha wapangaji na wamiliki wa jumba hilo, hauna dhamira mbaya isipokuwa ni kuokoa maisha ya watu na mali zao sambamba na kuzuia maafa yasiokuwa ya lazima.

Aidha alisema iwapo kutajitokeza tatizo lolote litakaloathiri maisha ya watu na mali zao kupitia jumba hilo bila ya shaka  mzigo mzito wa lawama itabebeshwa serikali.

Hivyo, alisema uamuzi wa kuwahamisha watu wote katika jumba hilo hauna mjadala mjadala kama wanavyotaka watu hao bali ni wajibu wao kufuata maagizo ya serikali ili kuepusha  vifo visivyo vya lazima.


Mkurugenzi wa Mkuu wa Mji Mkongwe, Issa Sarboko,alisema kwa mujibu wa ukaguzi wa kina uliofanywa na watendaji wa mamlaka hiyo, jumba hilo ni bovu na wakati wowote linaweza kuporomoka na  kusababisha mafaafa.

Alifahamisha kwamba miongoni mwa mambo yaliogunduliwa katika ukaguzi huo ambayo kama yataendelea kufumbiwa macho yataathiri maisha ya watu ni pamoja na dari jumba hilo kuwa katika hali mbaya kwa sababu kwa muda mrefu yaijafanyiwa matengenezo,kuvuja kwa paa na vyoo na kuta kufanya nyufa.

“Watumiaji walio wengi wa jumba hili hawajali hali hiyo kwa kuwa wamegeuza ghala za bidhaa zao huku wakisahau kama eneo lile linatumiwa na watu hivyo kama litajitokeza tatizo litawakumba watu wengi,”alisema.

Mkurugenzi wa Nyumba na Maendeleo na Makaazi, Ali Mwinyigogo, alisema kitendo cha kutohudhuria kwa walengwa si jambo la busara kwani kikao hicho ndicho kitachotoa fursa kwa wao kusikilizwa.

Alisema barua zilitolewa kwa wale wote ambao wamekuwa na mikataba halali lakini jambo la kusikitisha hawakufuata maelekezo ya wito na hatimae wameunda kamati ambazo hazitoweza kutimiza dhamira ya kikao hicho wakiwa wao peke yao.


Mmiliki wa mlango wa duka katika jengo hilo, Saleh Said Abdalla, alikiri jumba hilo ni bovu na kwamba uamuzi wa serikali wa kulivunja ni wa busara. 

Post a Comment

0 Comments