Mkuu wa Kampuni ya VIGOR Kamal Kanal akimkabidhi maji safi na salama Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika kambi kipindupindu Chumbuni.
Mkuu wa kambi ya wagonjwa wa kipindupindu iliopo Chumbuni Dkt. Ramadhani Mikidadi akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi mara baada ya kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika kambi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi akinawa mikono kwa maji yaliyotiwa dawa baada ya kuwatembelea wagonjwa katika kambi ya kituo hicho ili kujikinga na maradhi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mgharibi Abdallah Mwinyi akizungumza na madaktari wanaoshughulikia wagonjwa wa kipindupindu mara baada ya kuwaangalia wagonjwa waliolazwa kambini hapo.
(Picha Na Miza Othman-Maelezo Zanzibar).




1 Comments
Binadamu ,Leo namkumbuka sijuwi ni mwite mzee au vipi ,nikiwa kijana mdogo nasoma skuli ya darajani naishi Ngambo wakati huo mzee Abdallah Mwinyi akiwa ndio mkuuu wa duka ya michezo pale shangani ,kuna mwaka mmoja akaleta viatu viatu vitwavyo Inter lakini kama inavyokumbukwa siku zilikuwa maisha magumu lakini imani bado ilikuwapo kiasi fulani ijapokuwa pesa ilikuwa ngumu kuitumia katika mambo ya viyatu kama inter ,nikabahatika kwa matra ya kwanza kupata kiatu cha kuchumpa kutoka majuu ,leo nikimuangalia mzee Abdallah Mwinyi nimejaawa na huruma sikudhani hata siku moja maisha yatakuwa kama yalivyo sasa kwa upande wake
ReplyDelete