6/recent/ticker-posts

Kampuni ya Vigor yatoa msaada wa maji katika kambi ya kipindupindu Chumbuni

 Mkuu wa Kampuni ya VIGOR Kamal Kanal akimkabidhi maji safi na salama Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi  Abdallah Mwinyi kwa  ajili ya   wagonjwa waliolazwa  katika kambi kipindupindu Chumbuni. 
  Mkuu wa kambi ya  wagonjwa wa kipindupindu iliopo Chumbuni  Dkt. Ramadhani Mikidadi akitoa  maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi mara baada ya kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika kambi hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa  Mjini Magharibi  Abdallah Mwinyi  akinawa mikono kwa  maji  yaliyotiwa dawa  baada ya kuwatembelea wagonjwa katika kambi ya kituo hicho ili kujikinga na maradhi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mgharibi  Abdallah Mwinyi akizungumza na  madaktari wanaoshughulikia wagonjwa  wa kipindupindu mara baada ya kuwaangalia  wagonjwa waliolazwa kambini hapo.
           (Picha Na Miza Othman-Maelezo Zanzibar).

Post a Comment

1 Comments

  1. Binadamu ,Leo namkumbuka sijuwi ni mwite mzee au vipi ,nikiwa kijana mdogo nasoma skuli ya darajani naishi Ngambo wakati huo mzee Abdallah Mwinyi akiwa ndio mkuuu wa duka ya michezo pale shangani ,kuna mwaka mmoja akaleta viatu viatu vitwavyo Inter lakini kama inavyokumbukwa siku zilikuwa maisha magumu lakini imani bado ilikuwapo kiasi fulani ijapokuwa pesa ilikuwa ngumu kuitumia katika mambo ya viyatu kama inter ,nikabahatika kwa matra ya kwanza kupata kiatu cha kuchumpa kutoka majuu ,leo nikimuangalia mzee Abdallah Mwinyi nimejaawa na huruma sikudhani hata siku moja maisha yatakuwa kama yalivyo sasa kwa upande wake

    ReplyDelete