Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Karafu Ali Suleiman Musaa (mwenye kofia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ZSTC Ali Mohd wakimsaidia mama Maryam Ame wa Mkokotoni kuchambua karafuu walipofanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa karafuu wa Mkoa Kaskazini Unguja.
Karafuu zikiwa zimeanikwa kwa kutumia majamvi ambayo ni njia sahihi inayotakiwa na Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) katika kulinda hadhi ya Karafu za Zanzibar.
Mkulima wa zao la Karafuu wa Kiboje Vuai Seif Vuai akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Maafisa wa ZSTC walipofanya ziara ya kuwatembelea wakuli wa zao hilo katika maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru.
Mkulima wa Karafuu Khamis Jaku wa Mkwajuni akizungumza na Mkurugenzi wa Utawala na Mipango wa ZSTC Ussi Muhammed Juma na Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu Ali Suleiman Mussa walipowatembelea wakulima wa zao hilo katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru.
Maafisa wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar wakikusanya karafuu zilizoanikwa barabarani bila kutumia majamvi na kumtaka mwenye karafuu hizo na wakulima wengine kuacha tabia ya kuanika karafuu katika barabara kwani kunapunguza ubora wa karafuu hizo.
Picha na Ramadhani Ali Maelezo Zanzibar.





0 Comments