Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandis Cyprian
Luhemeja akishiriki mjadala kuhusu ‘Kutumia sayansi pamoja na maarifa ya asili
kwa ajili ya kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na
kuimarisha uhifadhi wa mazingira’, uliofanyika
pembezoni mwa Mkutano wa Saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA 7) unaoendelea
jijini Nairobi, Kenya Desemba 10, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandis Cyprian Luhemeja ameshiriki mjadala kuhusu ‘Kutumia sayansi pamoja na maarifa ya asili kwa ajili ya kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha uhifadhi wa mazingira’.
Mjadala huo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA 7) unaoendelea jijini Nairobi, Kenya Desemba 10, 2025.
Akiendelea kuchangia alieleza kuwa jamii hususan jamii za wenyeji wa pwani wamekuwa wakishirikishwa kikamilifu katika shughuli za ulinzi na uhifadhi wa matumbawe.
Akifafanua Zaidi, Mhandisi Luhemeja alifafanua kuwa mbinu ya kuishirikisha jamii imefanikisha wananchi kupata manufaa ya haki na yanayoonekana kupitia fursa za kipato zinazostahimili mbadiliko ya tabianchi.
Lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu, kushauriana na kuweka mikakati ya pamoja ya kujenga ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika ikolojia ya miamba ya matumbawe.
Mkutano huo unawashirikisha wakuu wa nchi na serikali, mawaziri wanaoshughulikia Mazingira, wataalam na wadau wa Mazingira na maendeleo endelevu kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na asasi za kiraia.
Aidha, Mkutano huu utajadili na kupitisha maazimio na maamuzi mbalimbali yanayohusu mabadiliko ya tabianchi, hifadhi ya bioanuai na udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira duniani.
Katika ufunguzi huo Naibu Waziri ameambatana na
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja, Balozi wa
Tanzania nchini Kenya ambaye pia ni Mwakilishi wa kudumu UNEP Mhe. Dkt. Bernard
Kibesse na Afisa Mazingira Mwandamizi Ofisi ya Makamu wa Rais Simeon Shimbe.



0 Comments