Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa
na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mhe. Mussa Zungu
pamoja na Viongozi na Wananchi mbalimbali wakishiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge
wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha
Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma leo tarehe 16 Desemba 2025.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa
na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mhe. Mussa Zungu
pamoja na Viongozi na Wananchi mbalimbali wakishiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge
wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha
Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma leo tarehe 16 Desemba 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akiweka udongo katika Kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, wakati wa Mazishi yaliyofanyika katika
Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.


Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
akizungumza na waombolezaji, mara baada ya Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo
la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha Ruanda
Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma tarehe 16 Desemba 2025.
Makamu wa Rais wa Jam huri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi amewaongoza waombolezaji kwenye Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa
Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha
Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma tarehe 16 Desemba 2025.
Akitoa salamu za rambirambi mara baada ya mazishi hayo, Makamu wa Rais amesema marehemu Jenista Mhagama alikuwa mtumishi wa kweli wa watu wake ambaye aliwatumikia na kuwajali.
Amesema Serikali, Wananchi na Chama cha Mapinduzi, wamepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake hautasauhaulika katika nyadhifa mbalimbali ambazo amewahi kutumika.
Makamu wa Rais ameongeza kwamba Serikali na Chama Cha Mapinduzi itaendelea kuenzi mchango wa marehemu Jenista Mhagana kwa kuendelea kuwa watetezi wa wananchi wa chini, ambapo ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali kuhakikisha wananchi wa hali ya chini ndio wanakuwa kipaumbele chao cha kila siku.
Aidha Makamu wa Rais amewasilisha salamu za shukrani za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozitoa kwa familia na wananchi wa Ruvuma kwa ujumla kutokana na maisha ya marehemu Jenista Mhagama. Amesema Rais Dkt. Samia ameguswa sana na msiba huo kutokana na mchango aliotoa marehemu Jenista Mhagama enzi za uhai wake.
Pia amewashukuru Viongozi wa Kanisa ambao wameshiriki katika Ibada mbalimbali zilizofanyika za kumuombea marehemu Jenista Mhagama kuanzia mkoani Dodoma hadi mkoani Ruvuma.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kumsimamia vema mkandarasi anayejenga barabara ya Kitai hadi Ruanda ili aweze kuendana na kasi iliyotarajiwa. Amesema tayari Serikali ilikwisha kutoa fedha za za ujenzi wa barabara hiyo kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo katika uchumi.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu ameishukuru Serikali,Bunge, Mawaziri, Wabunge, familia na wananchi wote kwa kujitoa na kuhakikisha Marehemu Jenista Mhagama anapumzishwa kwa heshima na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
16 Desemba 2025
Ruvuma.



0 Comments