6/recent/ticker-posts

Aliyemchoma kisu mke mwenza ahukumiwa miaka 20 Chuo cha Mafunzo

 Mahkama Kuu ya Zanzibar leo tarehe 30/01/2026 imemhukumu mshtakiwa Khadija Shabani Ali, mwenye umri wa miaka 35, mkazi wa Chukwani, Unguja, kutumikia kifungo cha miaka 20 chuo cha mafunzo.

Awali, mshtakiwa huyo alishtakiwa kwa kosa la kujaribu kuua, kinyume na Kifungu cha 193(b) cha Sheria Na. 6 ya mwaka 2018.
Ilielezwa kuwa mnamo tarehe 09/02/2025, majira ya saa saba mchana huko Chukwani, mshtakiwa alimchoma kisu katika paji la uso, shingoni, nyuma ya bega na kwenye vidole vya mikono ndugu Maymuna Said Suleiman, ambaye ni mke mwenziwe.
Akisoma maelezo ya hukumu, Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar, Mhe. Aziza Iddi Suwedi, amesema Mahkama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa, na hivyo kumtia hatiani mshtakiwa kwa kosa hilo.
Jumla ya mashahidi kumi (10) walitoa ushahidi wao Mahkamani.

Maimuna Said Suleiman aliyepigwa visu na mke mwenzake February mwaka jana 2025 amewaambia waandishi wa habari kwamba ameridhishwa na uamuzi wa Mahakama wa kumtia hatiani mke mwenzake Khadija Shaaban Ali wa kufungwa jela miaka 20 huku akitoa wito kwa wenye wake wenza kuacha tabia ya kuchukua sheria mikononi ambayo madhara humfikisha mtu asipotarajia akitoa mfano wa Khadija kwa sasa atawasumbua familia yake kumpelekea chakula huko alipo

Post a Comment

0 Comments