6/recent/ticker-posts

Taasisi za usajili wa huduma na ukusanyaji wa kodi zatakiwa kufanya kazi kwa pamoja



Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mhe. Rahma Kassim Ali, amezitaka Wizara na Taasisi za Serikali zinazohusika na usajili wa huduma na ukusanyaji wa kodi kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti na kuwabana wanaokwepa kodi ya matumizi ya ardhi, ambayo ipo kisheria.
Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau wa sekta husika, kilichofanyika Maisara katika Ukumbi wa Wizara
ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Mhe. Rahma alisema kuwa uongozi wa Wizara hiyo umefanya ziara katika maeneo mbalimbali na kubaini kuwepo kwa watu wengi wanaoendesha shughuli za kibiashara, ikiwemo biashara za utalii, bila kuwa na mikataba halali ya ardhi, huku wengine wakiwa na mikataba isiyosajiliwa.
Ameeleza kuwa tatizo hilo linawahusisha wageni pamoja na wananchi wazawa, ambapo baadhi yao hutumia mikataba ya mitaani kuwapatia wageni maeneo ya ardhi kwa njia zisizo rasmi, hali inayosababisha Serikali kukosa mapato halali.
Mhe. Rahma ameyataja maeneo yaliyoathirika zaidi na hali hiyo kuwa ni yale ya ukanda wa utalii, ikiwemo Paje, Jambiani na Mtende, na kusisitiza kuwa jitihada za Wizara yake pekee haziwezi kukabiliana kikamilifu na tatizo hilo bila ya ushirikiano wa dhati kutoka kwa taasisi zote zinazohusika.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, amesisitiza umuhimu wa taasisi za Serikali kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi, zitakazowezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Wakizungumza katika kikao hicho, maafisa kutoka Wizara na Taasisi husika wamesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazochangia hali hiyo ni kila taasisi kuzingatia malengo yake binafsi bila kuwa na msimamo wa pamoja katika mchakato wa usajili, utoaji wa huduma na ukusanyaji wa kodi za Serikali.
Kikao hicho, kimewahusisha maafisa kutoka Kamisheni ya Ardhi, Mamlaka ya Kodi Zanzibar (ZRA), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Kamisheni ya Utalii, BPRA pamoja na Tawala za Mikoa, kimeazimia kuunda timu ya pamoja itakayoratibu na kuunganisha jitihada


 

Post a Comment

0 Comments