6/recent/ticker-posts

amewataka Maafisa Vijana wa Wilaya kufanyakazi kwa ufanisi na kusimamia majukumu

Waziri wa Vijana ,Ajira na Uwezeshaji Mhe.Shaaban Ali Othman amewataka Maafisa Vijana wa Wilaya kufanyakazi kwa ufanisi na kusimamia majukumu yao ipasavyo ili kufikia malengo ya Serikali ya kuanzisha Wizara hiyo

Ameyasema hayo wakati wa ugawaji wa Vifaa mbalimbali vya kutendea kazi kwa Maafisa wa Maendeleo ya Vijana katika Wilaya za Unguja huko Ofisini kwake Mpendae Wilaya ya Mjini 

Amesema ugawaji wa Vifaa hivyo utasaidia ufanyaji wa kazi Kwa ufanisi katika mazingira yenye hadhi na staha jambo ambalo litachangia uwajibikaji na kufikia malengo ya uundwaji wa wizara hiyo

Aidha amewataka Maafisa Maendeleo hao kusimamia Uchaguzi wa Mabaraza ya Vijana katika ngazi za Shehia ili kupata Viongozi watakaokwenda na kazi ya Maendeleo .

 Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Ndugu Salama Mbarouk Khatib amesema Vifaa hivyo vimetumia gharama kubwa hivyo ni vyema watendaji kuvitunza na kuvifanyia kazi kwa ufanisi na kuwe na  huduma Bora zinapatikana .

 Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Vijana ShaibI Ibrahim Mohamed amesema watendaji wa Baraza la Vijana wa Wilaya walikabiliwa na changamoto ya vifaa Wizara iliona Iko haja kuwatafutia Vifaa ili kuimarisha sehemu zao za Kazi ili kwenda sambamba na mabadiliko ya wizara hiyo.

Nao Maafisa hao waliishukuru wizara hiyo na kuahidi kuvitunza Vifaa hivyo na kuifanyia kazi Kwa ufanisi na kuleta matokea chanya kiutendaji sambamba na kufuatilia Mabaraza ya Vijana kujua changamoto zao .

Vifaa vilivyokabidhiwa kwa Maafisa Maendeleo ya Vijana ni Meza ,Viti na Pikipiki na Vifaa kama hivyo vinatarajiwa kukabidhiwa kwa Wilaya zote za Pemba.










Imetolewa na Kitengo cha Habari.
WHSUM.

Post a Comment

0 Comments