6/recent/ticker-posts

Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar yaibukia London kutangaza Utalii


 Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar imeanza kampeni ya kutangaza vivutio vya kisiwa hicho kupitia mabasi maarufu ya London Buses.

Mji wa London unapokea watalii wakimataifa karibia milioni 20 kwa Mwaka, Soko kubwa ambalo Zanzibar inataka kulifikia. Kwa hiyo, Mabasi haya yatakayokuwa yakipita katika route ya Central London, eneo maarufu kwa Watalii, yataonyesha matangazo ya Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii, Arif Abbas Manji amesema "Kamisheni imeamua kuja na ubunifu huu wa kujitangaza ambao haujawahi kutokea katika historia ya Zanzibar ili kufikia watalii wengi zaidi kwa gharama nafuu zaidi."

Kampeni hio inatarajia kuanza rasmi Januari 21, 2026 na itazinduliwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Mbelwa Kairuki.

Post a Comment

0 Comments