Mkoa wa Mjini Magharibi. 17/01/2026.
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe, Dk. Riziki Pembe Juma amesema Serikali itaendelea kuimarisha Viwanja vya Michezo ili kuongeza hamasa ya Wananchi.
Ameyasema hayo wakati wa ugawaji wa Zawadi kwa Washindi wa mbio za Baskeli, zilizoanzia Mapinduzi Square Kisonge na kumalizia Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B.
Amesema Ujenzi na uimarishaji wa Miundombinu ya Michezo Nchini, imesaidia kuongeza shauku kwa Wananchi sambamba na kujenga Afya zao kiakili na kimwili.
Aidha Dkt. Riziki ameahidi kuwa Serikalii itaendelea kuwaenua Wanamichezo kupitia makundi yao, ikiwemo Michezo ya Asili kama vile Baskeli, Bao na Karata.
Nae Mkurugenzi wa ABM. Foundation Abdallah Idrissa Majura amesema lengo la kuandaa mashindano hayo ni kuendeleza Uridhi wa Mzanzibar ili usipotee.
Aidha Majura, ameiomba Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kuweka siku maalum ya mbio za Baiskeli sambamba na kuomba kuwasaidia kupata Ufadhili.
Kwa Upande wake Katibu wa Chama Cha Baskeli Zanzibar (CHABAZA) Saleh Kijiba Said ameipongeza Serikali kwa kuimarisha Miundombinu ya Barabara jambo ambalo limeondosha usumbufu wakati wa Mashindano na mazoezi.
Mashindano hayo, yamedhaminiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) na Mamlaka ya Ngorongoro (MCAA) ambapo jumla ya Wapanda Baiskeli 30 walioshiriki na kupatiwa zawaidi ya Fedha taslim.
Imetolewa na Kitengo cha Habari,
WHSUM
.jpg)
0 Comments