6/recent/ticker-posts

Taasisi ya Mobile Eyes ya Arusha yafanya kambi ya upasuaji wa maradhi ya macho kituo cha Afya Kizimkazi.





 Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Mobile Eyes ya Arusha kupitia ufadhili wa LIVING STONE CHARITABLE TRUST ya UK imefanya kambi ya upasuaji wa maradhi ya macho katika kituo cha Afya Kizimkazi.

Mratibu wa huduma za afya ya macho Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Fatma Juma Omar amesema upasuaji huo unafanyika kwa kuwafanyia uchunguzi wananchi wa Kizimkazi na kufanya upasuaji baada ya kugundulika kuwa na maradhi ya mtoto wa jicho.
Amesema kuwa katika kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kufanya kazi kituo hicho cha Afya Kizimkazi wameona ipo haja ya kutoa huduma hiyo kwa lengo la kuimarisha afya ya macho kwa wananchi kuwafanyia upasuaji huo.
Aidha amefahamisha kuwa ya katika kambi hiyo wagonjwa wapatao 135 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji baada ya kubainika kuwa na mtoto wa jicho kupitia wataalamu mbali mbali wa hapa nchini na nje ya nchi kwa mud awa siku nne .
Dkt Fatma ametoa wito kwa wananchi wote wa Unguja na Pemba kufika katika Hospitali na Vituo vya Afya pale zinapotokea fursa za kufanya uchunguzi wa maradhi mbali mbali yakiwemo ya macho ambapo kufanya hivyo kutasaidia kuondokana na upofu usio wa lazima kwa kupata tiba ya mapema.
Kwa upande wa Daktari wa macho kutoka Morogoro Dkt Ashraf Mlanzi amesema wameridhishwa na hatua ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kufanikisha miundombinu ya Afya iliyobora na ambayo inawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa kutokana na vifaa vilivyopo.
Amefahamisha kuwa tangu kuanza kazi yao hiyo wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji wananchi mbali mbali wenye matatizo ya mtoto wa jicho waliofika kituoni hapo kupata huduma hiyo na bado wanaendelea kuwapatia huduma na waliowapata wengi wao ni wenye mtoto wa jicho ambayo inasababishwa na umri na kuwataka kufika kupata matibabu ili kuzuiya upofu usiokuwa na lazima.
Kwa upande wa wananchi waliopata huduma ya kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kupata huduma hiyo ya matibabu ya mamcho na kuwataka wenye matatizo ya mamcho wanaposikia utoaji wa huduma kama hizo  kufika kituoni ili kuondokana na matatizo hayo.

Post a Comment

0 Comments