ZANZIBAR
WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kushirikina na Taasisi yaWorld Medical Color ya nchini Italy katika kuimarisha huduma za Afya kwa upande wa Ultrasound kwa kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake ili waweze kufanya matibabu kwa ufanisi.
Akizungumza mara baada ya kuwatunuku vyeti vya kumaliza mafunzo ya Ultrasound wataalamu kutoka vituo vya Afya Unguja na Pemba Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema kuwa wataalamu hao watasaidia kutoa huduma hasa kwa mama wajawazito pamoja na dharura mbali mbali ambazo zinazohitaji Utrasound.
Amefahamisha kuwa kuwepo kwa wataalamu wa Utrasound katika vituo vya Afya kutasaidia kuepusha kwenda kufata huduma hiyo Hospitali ya Wilaya na Mkoa kwa ajili ya kukosa huduma ya Ultrasound katika vituo hivyo.
Aidha amesema wanaendelea kushirikina na World Medical Color kuwapatia mafunzo wataalamu mbali mbali wa afya ili kutoa huduma ya Ultrasound kwa umakini katika sehemu zao za kazi na kuhakikisha wanaengeza ufanisi wa huduma hiyo.
Dkt Amour ametoa wito kwa wataalamu hao kuhakikisha kwamba wanaporudi katika maeneo yao ya kazi wanatoa huduma kwa kuzingatiamaadili ya kazi zao na kuhakikisha kwamba wanaofika katika vituo vyaovya Afya wanaridhika na huduma hizo ili kuondoa changamoto zamalalamiko kwa wananchi.
Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya World Medical Color Profesa Franca Mellem amesema wataendelea kushirikiana na Sekta ya Afya Zanzibar katika kuhakikisha huduma ya Ultrasound inakuwa kwa kiasi kikubwa katika mahospitali na vituo vya Afya.
Amefahamisha kuwa wataendelea kuwapatia ujuzi wa matumizi ya Ultrasound wataalamu wa Zanzibar ili kuhakikisha wanaleta matokeo mazuri ya uchunguzi kwa mama wajawazito na wenye matatizo mengine na kupatiwa matibabu kwa haraka.
Kwa upande wa Mkufunzi na Mtaalamu wa huduma za Uchunguzi waUtrasound Wizara ya Afya Zanzibar Khamis Abdulrahmn Simai amesema kuwa jumla wanafunzi wapatao 14 wamefaulu mafunzo yao kati ya wanafunzi 20 na wanafunzi 6 watarudia mitihani yao mwezi wa sita mwaka huu ili kumalizia masomo yao
Aidha amefahamisha kuwa mafunzo ya Ultrasound yameanza tangu mwaka 2006 hapa nchini ambapo hiyo ni awamu ya nne na kusisitiza kuwa wafanyakazi wengi wanaofanya huduma hiyo ni matunda kupitia World Medical Coler ambao ndio waliowapatia mafunzo hayo.
Kwa upande wa wahitimu wa mafunzo hayo Abdulla Amir Salum kutoka Kituo cha Afya Kidimni na Sabiha Soud Mohamed kutoka Kituo cha Afya Michenzani wamesema mafunzo yao wameanza tangu mwaka 2023 na yatawasaidia katika kuimarisha huduma za afya katika sehemu zao za kazi.
Wamefahamisha kuwa watahakikisha kuwa wanasaidia jamii juu ya huduma hiyo kwa lengo la kuondokana na wananchi kwenda kufata huduma hiyo katika hospitali za Wilaya ama Mkoa.


0 Comments