Picha katika matukio ni Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil akifanya ziara katika ofisi kuu za Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF), Michenzani Mall Wing “C” Ghorofa ya 4 Unguja leo 26/01/2026. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuona utendaji wa kazi za ZHSF.
Aidha, Mheshimiwa Waziri alipata fursa ya kutambulishwa kwa viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZHSF, Menejimenti ya Mfuko, pamoja na kufahamu kazi za Idara na Vitengo vya Mfuko.
Hatahivyo, Uongozi wa ZHSF ulifafanua mafanikio, changamoto na mipango ya baadae ili kufikia lengo la afya bora kwa wote. Vilevile Mheshimiwa Waziri alipongeza ZHSF kwa hatua iliyofikiwa katika usajili wa Sekta isiyorasmi na makundi mengine.
“Afya Bora kwa Wote”
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano wa Umma,
Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar


0 Comments