Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria
uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea mafuta katika Bandari
ya Dar es Salaam katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam, tarehe 03
Machi, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan akisikiliza maelezo ya Mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea Mafuta
katika Bandari ya Dar es Salaam, Kigamboni Jijini Dar es Salaam, tarehe 03
Machi, 2026. Ujenzi wa Matanki hayo utasaidia kupunguza uhaba wa mafuta nchini,
kupunguza muda wa meli kusubiri nangani kutoka wastani wa siku 22 hadi siku 7,
kupunguza muda wa kushusha shehena ya mafuta kutoka siku 7 hadi siku 1,
kuongeza mapato ya Taifa pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan mara baada ya kuweka jiwe la msingi Mradi wa Ujenzi wa Matanki ya
kupokea Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kigamboni, Jijini Dar es Salaam,
tarehe 03 Machi, 2026.
Muonekano wa eneo la Mradi
wa ujenzi wa Matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam,
Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa Matanki hayo utasaidia kupunguza au
kuondoa kabisa uhaba wa mafuta Nchini, kuimarisha usalama wa nishati hiyo,
kupunguza muda wa meli kusubiri nangani kutoka wastani wa siku 22 hadi siku 7,
kupunguza muda wa kushusha shehena ya mafuta kutoka siku 7 hadi siku 1,
kuongeza mapato ya Taifa kupitia makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali zitakazo
kusanywa na Mamlaka husika pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania
.jpeg)



0 Comments