Mnamo tarehe 1 Machi 2026, Taasisi ya Benki za Kiislam na Fedha (IIBF) kupitia Umoja aa Wanafunzi wa Tahasusi hiyo @zuibfa_znzuniversity (ZUIBFA), wameandaa Iftar ya pamoja sambamba na Kongamano Maalum lililojadili kwa kina nafasi na mchango wa wanawake katika uchumi wa Kiislamu.
Tukio hili muhimu liliwakutanisha wadau kutoka sekta ya taaluma, serikali pamoja na sekta binafsi kwa lengo la kuimarisha uhusiano mwema, ushirikiano wa kitaasisi, na mshikamano katika kukuza maendeleo ya uchumi unaozingatia misingi ya Kiislamu.
Kwa udhamini wa PBZ Bank na ZIC Takaful, kongamano hilo lilionesha dhamira ya wadau hao kuendelea kuunga mkono elimu ya fedha za Kiislamu pamoja na uwezeshaji wa vijana katika kujenga mustakabali endelevu wa kiuchumi.
Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Mheshimiwa #Salama_Mbarouk_Khatib, aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Vyama vya Ushirika, Bi. #Zainab, aliwasilisha dira ya Wizara kuhusu azma ya kuanzishwa kwa Benki ya Ushirika itakayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi, huku akipendekeza ushiriki wa wanafunzi wa ZUIBFA katika kuendeleza mpango huo kama sehemu ya kujenga ushirikiano wa kimkakati kati ya elimu na utekelezaji wa sera.
Aidha, Balozi #Abdulswamad_Abdulrahim aliahidi kutoa malezi na msaada kwa vijana kupitia programu za mwongozo na ushirikiano zitakazofungua fursa mpya za maendeleo.
Iftar ya pamoja imeendelea kudhihirisha nafasi ya @zanzibar_university_zu kama kitovu cha maarifa, maadili, na ubunifu katika kujenga uchumi jumuishi na endelevu unaowanufaisha wote.



0 Comments