6/recent/ticker-posts

Idara ya Elimu Sekondari yaandaa Mashindano ya sayansi na ubunifu



Katika kuhamasisha Wanafunzi kuyapenda masomo ya Science, Technology, Engineering na Mathematics (STEM) Idara ya Elimu Sekondari kupitia programu ya BGSLP imeandaa mashindano kwa Wanafunzi yaliyofanyika Skuli ya Limbani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mashindano ya sayansi na ubunifu kupitia programu ya BGSLP. Lengo ni kuongeza hamasa kwa wanafunzi kuyapenda na kuyasoma masomo ya STEM, Science, Technology, Engineering na Mathematics. Jumla ya skuli sita zimeshiriki tatu Wilaya ya Wete na tatu Wilaya ya Micheweni.

Katika mashindano hayo Wanafunzi wamepata fursa ya kuonesha vipaji vyao kupitia Ubunifu ulio wakilishwa kwa njia ya ushindani.

Wanafunzi  wameishukuru Serikali  kwa kuwaletea mradi huo  wenye lengo la kuwajengea moyo  wa kuyapenda  zaidi Masomo ya Sayansi.

Wanafunzi Walioibuka Washindi katika Mashindano hayo Wamewataka wanafunzi ambao hawaku bahatika kupata nafasi ya kwanza wasikate tamaa badala yake wazidi kupambana kwa lengo la kupata nafasi za mwanzo katika ubunifu wao.

Post a Comment

0 Comments