Hayo ameyasema mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni bi Hafsa Aboud Talib mara tu alipofanya kikao na viongozi wa Jumuiya ya Skuli za Binafsi ( ZAPS)
Bi Hafsa amewasisitiza viongozi hao kushajihisha skuli za binafsi kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo na utamaduni kwa lengo la Kibona na kukuza vipaji vya wanafunzi wanaosoma skuli za binafsi.
Walimu wasijaribu kuuwa vipaji vya wanafunzi kwa sababu ushiriki wa michezo kwa mwanafunzi ni jambo la muhimu kwa sababu ya kuchangamsha akili zao, kujenga afya lakini pia michezo ni fursa.
Bi Hafsa ametoa mifano tafauti ya veterani ambao walipokuwa wanafunzi walishiriki michezo mbalimbali ali WEMA FEI TOTO hali ambayo kwa sasa imewasaidia kukuza uchumi wa nchi pamoja kukabiliana na maisha yao binafsi kwa sababu michezo ni fursa lakini pia ni ajira.
Viongozi hao wameahidi kukaa pamoja na uongozi wa skuli mbalimbali za binafsi kwa lengo la kuimarisha michezo katika sekta ya elimu lakini pia kuweza kufahamu na kuviimarisha vipaji vya wanafunzi ili kuendana na mabadiliko ya mitaala ambayo yanamwezesha mwanafunzi aweze kujitegemea mara tu anapomaliza elimu yake ya lazima.
Imetolewa na kitengo cha habari - WEMA

0 Comments