ZASISITIZA USHIRIKIANO MAENEO YA UTAALAMU,
UZOEFU
Naibu
Katibu Mtendaji Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Juma
Msafiri Karibona amehimiza suala la ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya
Tume hiyo kwa ofisi za Unguja na Pemba.
Bw.
Karibona aliyasema hayo ofisi za Tume zilizopo Mombasa, Wilaya ya Magharibi B
Mkoa wa Mjini Magharibi alipozungumza katika kikao cha pamoja
kilichowashirikisha watumishi wa THBUB ofisi ya Unguja na Pemba kwa njia ya
mtandao (zoom meeting).
Aidha,
Bw. Karibona alisisitiza ushirikiano zaidi katika kubadilishana uzoefu na
utaalamu huku akiisifia THBUB ofisi ya Pemba kupiga hatua zaidi katika
kutekeleza majukumu yao ikiwemo ufunguzi wa klabu za haki za binadamu katika
taasisi za elimu kwa skuli na vyuo vya kati pia kufanikiwa kutembelea maeneo
ambako watu huzuiliwa kama vituo vya kulelea watoto yatima na kufanya vipindi
mbalimbali katika vyombo vya habari ili kuifikia jamii kwa haraka na kuwapa
elimu ya Haki za Binadamu na Ukiukwaji wa Misingi ya Utawala Bora.
Katika
hatua nyengine Bw. Karibona alimsihi Mfawidhi wa ofisi ya Pemba Bw. Suleiman
Salim Ahmad, kuwatumia wataalamu waliopo ofisi ya Unguja na kuangalia namna
bora ya kuboresha bajeti za ofisi hizo.
Alisema,
licha ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa na ofisi mbili hizo ikiwemo ongezeko la
rasilimali watu kutoka wafanyakazi nane hadi 26 kwa ofisi ya Unguja na Pemba
kutoka wafanyakazi wawili hadi wafanyakazi nane.
Pia
Bw. Karibona alitaja maeneo muhimu zaidi ya kuimarisha ushirikiano wao ni eneo
la Elimu kwa Umma na masuala ya habari, Utumishi, Utawala, Uhasibu na eneo la
Mipango.
Naye,
Mfawidhi wa THBUB ofisi ya Pemba Bw. Suleiman Salim Ahmad alikiri kuwa Pemba
imeitangulia Zanzibar katika utekelezaji wa kazi zao ikiwemo ufunguzi wa klabu
ambapo kwa sasa tayari wameshafungua klabu 15 za Haki za Binadamu kwa taasisi
za elimu zikiwemo mbili kwa skuli za msingi, saba Sekondari na sita kwa vyuo
vya kati.
Aidha,
viongozi wawili hao wamekubaliana kuimarisha bajeti za ofisi zao katika
kuwatumia wataalamu waliopo Unguja na kuendeleza utendaji kazi wa ofisi za Tume
kisiwani Pemba.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

0 Comments