MENEJA Masoko wa ZANTEL Mohammed Mussa Baucha akimkabidhi Vitabu Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar Sichana Haji Fumu, kwa ajili ya matumizi ya Maktaba hiyo.ikiwa ni Vitabu alivyotunga Profesa Abdulrazak Gurnah, makabidhiano hayo yamefanyka katika Maktaba Kuu Maisara.
VITABU vya Muandishi Profesa Abdulrazak Gurnah, Mzanzibari anayeishi Nchini Uingereza vilivyotolewa Msaada na Kampuni ya Simu ya ZANTEL vyenye thamani ya shillingi laki tatu kwa ajili ya matumizi ya maktaba kuu Zanzibar.
MENEJA Masoko wa ZANTEL Mohammed Mussa akitowa changamoto kwa Wanafunzi wa Skuli mbalimbali waliohudhuria Mhadhara huo kuandika Insha kutokana na Muandishi huyo na elimu walioyopata na Kampuni yake kuahidi kutowa zawadi kwa Mshindi wa Kwanza na Wapili wa Isha hiyo.
PROFESA Abdulrazak Gurnah akitowa muhadhara wa vitabu vyake alivyovitunga kwa Wanafunzi na Wananchi waliohudhuria Mhadhara huo uliofanyika ukumbi wa Makataba Maisara
MAOFISA wa ZANTEL wakifuatilia Mhadhara huo ambnao ulidhaminiwa na Kampuni hiyo ya Simu za Mkononi ZANTEL.
PROFESA Abdulrazak Gurnah akitowa maelezo wakati akisomo kimoja ya vitabu vyake katika Mhadhara ulioelezea utunzi wake wa vitabu Nchi Uingereza
WANAFUNZI wa Skuli mbalimbali wakifuatilia maelezo anayoyatowa Profesa Abdulrazak katika ukumbi wa Maktaba Kuu Zanzibar.
MSHAURI wa Wizara ya Elimu Zanzibar Mohammed Gurnah akitowa maelezo ya mafanikio ya Mtunzi huyo walipokuwa wakisoma Skuli
ABASS Mussa akichangia uhaba wa vitabu katika maktaba zetu
BAADHI ya Wananchi wakimsikiliza Profesa Abdulrazak akitowa maelezo yake na mafanikio yake katika utunzi wa Vitabu mpaka sasa ameshatowa vitabu saba,
MWANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari ya Laurent Barke Salah akichangia jinsi ya Wanafunzi wengi hawapati kuchukua vitabu kujisomea
MWANAFUNZI Bilal Hussen wa Skuli ya Kidongochekundu kidatu cha nne
PROFESA Abdulrazak akifafanua jambo katika Mhadhara huo uliondaliwa na Kampuni ya simu ya ZANTEL.
MWANAFUNZI wa Skuli ya Nyuk Daniel Sabastian wa Kidatu cha Sita akichangia jinsi wanafunzi wanawezaje kufikia kiwango kama chake cha kuweza kutunga Vitabu. na alitaka mihadhara kama hii wafanyiwe na watoto wa skuli za msingi ndiko kwenye chimbuko la elimu.
MWANANCHI Mohammed Yussuf akichangia katika mhadhara huo wa Profesa Abdulrazak.MUANDISHI wa Star TV Munir Zakaria akichangia katika mdahalo huu jinsi baadhi ya waandishi wa Vitabu vitabu vyao haviweke kufundishia watoto skulini..
Nimesikia habari kuwa huyu Gurnah ni Sahib na mpenzi mkubwa wa Salman Rushdie na maandishi yake. Salman Rushdie ni yule Mwingereza alieandika kitabu kilichomkashifu mtume (SAW). Kama bado yupo Unguja atakaepata nafasi hebu amuulize kama kweli ni rafiki wa Salman Rushdie na kama anavipenda vitabu vyake hasa kile cha "Satanic Verses"
ReplyDelete