Khamis Juma
MVUVI mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Hamid Mahawi (38), mkazi wa Kivunge, amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akiwa baharini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mselem Masoud Mtulia alithibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo alibainisha kutokea katika bahari ya wilaya ndogo ya Tumbatu.
Alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 juzi asubuhi ambapo katika chombo hicho kilichobeba wavuvi watano, kilipigwa na radi na marehemu huyo alianguka chini ya bahari.
Alisema wenziwe waliweza kurudi juu kwa masaada, ambapo mwili wa marehemu huyo ulisaidiwa kuokolewa na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).
Baada ya kuokolewa mwili huo ulifanyiwa uchunguzi kabla ya kukabidhiwa jamaa zake kwa hatua za mazishi.
Katika tukio hilo, Sheha Khamis Mcha (21), mkaazi wa Matemwe yeye amejeruhiwa katika tukio hilo na kulazwa hospitali ya Kivunge.
No comments:
Post a Comment