Habari za Punde

SIKILIZA MEZA DUWARA - REDIO UJERUMANI LEO

Katika kipindi cha "MAONI Mbele ya Meza ya Duwara" cha Radio Deutsche Welle kutoka Ujerumani, ambacho kitatangazwa LEO, jumamosi mchana ( April 30, 2011 ), punde baada ya Taarifa ya Habari za Ulimwengu ya saa saba za mchana kwa saa za Afrika Mashariki, mada itakayozungumziwa ni juu ya miaka 47 ya Muungano wa Tanzania, kero zinazotajwa katika Muungano huo na mustakbali wake. Kipindi hicho kitarejewa kwa upana zaidi jumapili ijayo, tarehe Mosi Mei, 2011, punde baada ya Taarifa ya Habari za Ulimwengu ya saa 12 jioni, saa za Afrika Mashariki.

Watakaoshiriki na kutoa maoni yao ni waziri wa zamani wa serekali ya Mapinduzi na pia serekali ya Muungano, Bwana Hassan Nassor Moyo; mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bwana Kabwe Zuberi Zitto; msemaji wa kundi la Wazanzibari walioko ng'ambo- katika nchi za Skandinavia, Dr. Yusuf Saleh Salim; na Profesa Julius Nyang'oro wa Chuo Kikuu cha Mkoa wa Carolina ya Kaskazini, Marekani, ambye pia ni mwandishi wa kitabu juu ya maisha ya Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Tega sikio wakati huo ili upanuwe mawazo yako juu ya Muungano wa Tanzania.

Nakutakia usikilizaji mzuri.




Ahsante.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.