Habari za Punde

DK SHEIN AMTEUA ABDULLA SULEIMAN ABDULLA - MWENYEKITI MPYA BARAZA LA CHUO CHA UTAWALA WA UMMA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MApinduzi Dk Ali Mohamed Shein amemteua Abdulla Suleiman Abdulla kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la chuo cha utawala wa umma Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa uwezo aliopewa na chini ya kifungu 5(3) cha sheria ya chuo cha utawala wa umma  nambari 1 ya 2007

Kabla ya uteuzi huo, nd Abdulla alikuwa mkuu wa shirika la mpango wa chakula (WFP) katika wizara ya kilimo Zanzibar. Pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Mipango ya Maendeleo na Sera iliyokuwa chini ya Wizara ya fedha na mipango.

Nd Abdulla ana shahada ya Chuo Kikuu na uteuzi huu umeanza tarehe 25 Mei 2011.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.