KIBAJAJI cha kubebea Wagonjwa kilichotolewa na Mbunge wa Jimbo la Fuoni, Said Zuberi kikiwasili katika viwanja vya Skuli ya Fuoni kwa kukabidhiwa Jumuiya ya Maendeleo ya Fuoni, katika Uzinduzi wake.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Seif Iddi akimkabidhi funguo Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Fuoni Ally Abdulrahim, kwa ajili ya Jimbo hilo kutowa huduma za Kwanza kwa Wagonjwa ili kutowa usafiri wa kuwapeleka Hospitali.
MAMA Asha Balozi Seif Iddi akisalimiana na Viongozi wa Jumuia hiyo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika viwanja vya Skuli ya Fuoni.
WASOMA utenzi wakisoma katika sherehe za Uzinduzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Fuoni.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Iddi akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Jimbo la Fuoni katika uzinduzi wa Jumuiya yao uliofanyika katika Viwanja vya Skuli ya Fuoni kulia Afisa Tawala wa Wilaya ya Magharibi Ali Mohammed Ali na Mbunge wa Jimbo la Fuoni Said Zuberi.
WANANCHI wa Jimbo la Fuoni wakishuhudia Uzinduzi wa Jumuiya yao, wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake kwao.
MBUNGE wa Jim,bo la Fuoni Said Zuberi akitowa Historia fupi ya Jumuiya hiyo wakati wa Uzinduzi wake katika viwanja vya Skuli ya Fuoni
WANANCHI wa Jimbo la Fuoni wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake katika Uzinduzi wa Jumuiya ya Maendeleo Fuoni iliozinduliwa na Mama Asha Balozi.
MSOMA Salama Bakari Wakati akisoma risala ya Jumuiya kwa mgeni rasmi katika Uzindizi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Fuoni.
MDAU hivi ndivyo iliovyokuwa katika uzinduzi wa Jumuiya ya Maendeleo Fuoni, Mtoa ishara kwa Watu wasiosikia akitowa ishara kuashiria maneno yanaosemwa ili kufahamu Watu wasiosikia.
MKE wa Makamu Pili wa Rais Zanzibar Mama Asha Balozi akihamashisha Wananchi wa Jimbo la Fuoni kuchangia Jumuiya yao, Baada ya yeye kuchangia dola 300/= taslim katika uzinduzi huo jumla ya shilingi 720,000 na Dola 750 zimechangwa katika harambe hiyo.
MKE wa Makamu wa Rais wa Zanzibar akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Fuoni Said Zuberi akiwahamashisha Wananchi wa Jimbo hilo chungia jumuiya yao.
No comments:
Post a Comment