Habari za Punde

TAMASHA LA WASANII BORA WA MWAKA ZANZIBAR - ZANZIBAR MUSIC AWARDS

 MSANI Bora wa Mwaka 2010 Bi, Mwapombe Hiyari akishindikizwa na Mstaafu Meya Mahboud Juma  kupanda jukwaani kuchukuwa Tuzo yake.  
 NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Issa Haji  Ussi Gavu akimkabidhi Tunzo ya Msanii bora wa Mwaka 2010 Bi Mwapombe Hiyari, katikati Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation Limited. akishuhudia Meya Mstaafu Mahboub Juma, tunzo hizo zimetolewa katika Ukumbi wa Salama Bwawani.    
MAMBO ya Tunzo za Wasanii bora wa Mwaka 2010, na kuibuka Msanii wa Mwaka Bi. Mwapombe Hiyari ameibuka kuwa msanii wa Mwaka, akikabidhiwa tunzo yake na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Issa Haji Ussi Gavu..   
 MSANII wa Mwaka 2010  Bi Mwapombe Hiyari  akiwa na Tunzo yake baada ya kukabidhiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani.  
 NAIBU Waziri  wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi Gavu akimkabidhi Tunzo Mkurugenzi wa Kampuni ya Zanzibar Media Corporation, muandalizi wa Tamasha hilo,  
 DJ Sam kulia na DJ G love wakiwa ndani ya Nyumba  wakati wa Tamasha la Tunzo za Wasanii Bora wa Mwaka 2010  
WADAU   wa muziki wakifuatilia  utoaji wa Tunzo za wasanii bora wa mwaka 2010 katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawni.   
 
MKURUGENZI  Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar  ( ZBC ) Hassan Mitawi  akimkabidhi Tunzo ya Wimbo Bora kwa Taarab ya ' Wimbo wa kufuru itakudhuru' Kisasa Kikundi cha Zanzibar One, akipokea muimbaji wa Kikundi hicho.      
MSANII wa Zanzibar One akitowa shukrani kwa wapenzi wao  kwa kuwapigia kura na kuibuka Msindi wa Wimbo Bora wa Taarab ya Kisasa.  
 MTANGAZAJI wa Redio ya  Zenj FM Issa Salum akifanya vitu vyake katika Tamasha la  kuwazawadia Tunzo Wasanii Bora  iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani.
 KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Zanzibar   Jamal Kassim Ali  (kulia) akimkabidhi Tunzo Msanii  Bora wa Kiume Taarab ya Kisasa Mwaka 2010  Issa Kassim kutoka kikundi cha Diamond Taarab  cha JKU.    
MSANI Issa Kassim akiwa na tunzo yake ya Msanii wa Kiume wa Taarab ya Kisasa, baada ya kukabidhiwa tunzi hiyo akipozi kwa kuraha ya pekee.  
 MSANII wa Kikundi cha Malindi Taarab Cholo Ganuni akipokea Tunzo ya Taarab Asilia  iliyochukuliwa na  Kikundi hicho cha Malindi Muziki Taarab kwa Mwaka 2010.   
 MEYA Mstaafu Mahboub Juma kulia akimkabidhi Tunzo ya Msanii Bora wa Taarab Asilia Iddi Suwed, kutoka Kikundi cha Culture Taarab ikipokelewa kwa niaba  na Taimur. Lukuni.     

MDAU wa  kituo cha Televisio cha Zanzibar Cable Masoud Kibonge ACHUDI akiwa makini kuchukuwa kila tukio  katika Tamasha la Wasanii Bora wa mwaka 2010 iliofanyika ukumbi wa Salama Bwawani.


 WASANII wa Kizazi Kipya wakitowa burudani katika Tamasha la Wasanii wa Bora mwaka 2010.

MKURUGENZI wa Zanzibar Media Corporation  Mohammed Seif Khati akimkabidhi CD ya Wasanii wa Tunzo ya Bora wa mwaka 2010 Mgeni Rasmin wa Tamasha hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Issa Haji Ussi Gavu. 
WADAU wa Kituo cha Television cha Zanzibar Cable  wakihakikisha  Wananchi wanapata burudani kupitia katika Luninga zao mahome.  
MKE wa Mkurugenzi wa ZBC Brigitte Mitawi akimkabidhi Tunzo ya Msanii Bora Sultan King 
MSANII wa Kizazi Kipya Sultani King akiwa na Wapambe wake Jukwaani baada ya kukabidhiwa Tunzo yake akitowa shukrani kwa Wapenzi wake.
AFISA wa Benki ya Biashara ya Kenya Tawi la Zanzibar KCB  Abdull Mshangama  akimkabidhi  Tunzo ya  Mshairi Bora  kwa Mwaka 2010, Omar Ramadhani.   
MKURUGENZI wa Kikundi cha Taarab cha Zanzibar One  Abdalla Ali (DUU) kulia akipokea Tunzo ya Albam Bora kwa mwaka 2010 'Albam ya kufuru itakuzuru'  kutoka kwa Afisa wa Benki ya Exim Gabriel.
MKURUGENZI wa Zanzibar One Taraab  Abdalla Ali DUU akiwa na Tunzo yake ya Albam Bora ya Kufuru itakuzuru, kwa mwaka 2010.
WASANII wa Zanzibar Onae Taarab wakiwa na Tunzo yao baada ya kukabidhiwa katika Tamasha la Wasanii Bora. 

MKURUGENZI wa Zanzibar Media Corporation  na Mbunge wa  Uzini  Mohammed Seif Khatib , akimkabidhi Msanii Bora wa Kike Taarab Asilia Saada Mohammed.

MSANII wa Tarab Asilia kwa mwaka 2010 Saada Mohammed akiwa na Tunzo yake baada ya kukabidhiwa.  

MSANII wa Kizazi Kipya  Baby J. akitowa burudani katika Tamasha la Wasanii Bora wa Mwaka 2010, katika Ukumbi wa Salama Bwawani   
BABAY .J  akifanya vitu vyake katika Tamasha la Wasanii Bora   
WAHESHIMIWA wakifuatalia Tamasha la Wasanii Bora wa Mwaka 2010 katika ukumbi wa Salama Bwawani kutoka kulia Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Abdillah Hassan Jihad, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi na Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation na Mbunge wa Uzini Mohammed Seif Khatib. 
MWENYEKITI  Breeze Fm Redio -Tanga, Aisha Kigoda akimkabidhi Tunzo Msanii Chipikizi wa Kike Nasma Nassor kwa wimbo wake 'INATOSHA'.   
MSANII Chipukizi wa Kizazi Kipya Nasma Nassor , akiwa na Tunzo yake  baada ya kukabidiwa.
AFISA wa Kampuni ya Usafiri ya Azam Marine Abrazak kushoto akimkabidhi Tunzo ya Msanii Chipukizi wa Kikume Mantuzo na wimbo wake wa 'NATAMANI' 
MSANII Chipukizi wa Kiume Mantuzo, akiwa na Tunzo yake baada ya kukabidhiwa.




WADAU wa Muziki wakishangilia Washindi wa Tunzo za Wasanii Bora wa mwaka 2010, wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani.wakishughudia Tamasha hilo. 
MENEJA wa Zenj Fm Saidi Khamis akimkabidhi Tunzo Msanii Bora wa Kike 2010 Baby J. 
MSANII Bora wa Kike wa Muziki wa Kizazi Kipya Baby J. akiwa na Tunzo yake.
MKURUGENZI wa Bomba Fm Gulu Ramadhani akimkabidhi Tunzo ya Studio Bora ya Mwaka 2010 ya Six Record Said Aboud.
MMILIKI wa Studio Bora kwa Mwaka 2010 Six Record  Said Aboud akipozy na Tunzo yake. 
MEYA Mstaafu Mahboub Juma na Meya wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib wakifuatilia Tamasha la Wasanii Bora wa Mwaka 2010 katika Ukumbi wa Salama Noteli ya Bwawani. 
Afisa Mauzo wa  Vodacom  Mohammed Mansoor  kushoto akimkabidhi Tunzo ya Mwanamuziki Bora wa Mwaka 2010 Cholo Ganuni  katika Tamasha la kwazawadia Tunzo Wasanii bora wa  2010.

MSANII Cholo Ganuni akitowa shukrani kwa wapenzi wake kwakumuwezesha kutowa Tunzo hiyo.

MSANII Sultani King akitowa burudani katika Tamasha la kuwazawadia Tunzo Wasanii Bora wa Mwaka 2010 katika Ukumbi wa Salama Bwawani.  

MASHABIKI wakimshangilia Sultan King akitowa burudani Ukum,bi hapo.
MENEJA Masoko wa Vodacom Zanzibar Mohammed Mansoor a kimkabidhi Tunzo Msanii Bora wa Kiume Juma 20 kwa mwaka 2010.
SANII Bora wa Kiume kwa Mwaka 2010 Juma 20, akiwa na Tunzo yake. 

 MEYA wa Mji wa Zanzibar Khatib Abrahaman , kushoto akimkabidhi Tunzo ya Msanii wa Wimbo Bora kwa mwaka  2010 Msanii Sultan King .




MSANII Sultan Kingi akipozi na Tunzo yake Jukwani baada ya kukabidhiwa katika Tamasha ola Wasanii Bora wa mwaka 2010. 
MASHAROBARO  wakimshangilia Sultan King akitowa shukrani zake kwa Wapenzi wake waliompigia kura.
 WAZIRI wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo Abdilah Hassan Jihad akimkabidhi Tunzo ya Ngoma Asilia Kikundi cha Darati Mchiriku, Ali Khamis Darati.baada ya kukindi chake kushinda Tunzo hiyo.




MSANII Ali Khamisi Darati akiwa na Tunzo yake Jukwaani
MSANII wa Ngoma Asili ya Mchiriku Ali Khamis Darati akiwa na wapambe wake Masharobaro Jukwaani akitowa shukrani zake kwa Wapenzi wake waliompa bigup.

2 comments:

  1. Safi zenji naona mnakuja kwa kasi, kaka Mapara najua umebanwa na kazi ila ingekua poauungetuekea Majina kwa kila picha inakua vyema zaidi. Honera kwa kazi

    ReplyDelete
  2. Thnx kwa maelezo, at least i got something

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.