Habari za Punde

SPIKA MAKINDA AKERWA NA WABUNGE WANAOSINZIA

Na Happiness Mtweve,Dodoma

SPIKA wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema kuwa anakerwa na wabunge wanaosinzia wakiwa bungeni na badala yake anafurahishwa na uchangamfu unaoonyeshwa na wabunge hivi katika bunge hili la kumi.


Makinda alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati wa chakula cha jioni na waandishi wa habari katika ukumbi wa Dodoma hoteli kilichoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za bunge BUPAT.

Spika alisema kuwa bunge hili linamabadiliko makubwa kutokana na changamoto mbalimbali zinazotolewa na waheshimiwa wabunge hivi sasa na kulifanya bunge kuwa na uchangamfu mkubwa.

"Jamani nyie waandishi hebu semeni ukweli bunge halina mabadiliko yeyote alihoja makinda.

Alisema kuwa hafurahishwi hata kidogo na wabunge wanaosinzia bungeni kwani bunge likikosa uchangamfu linakuwa halipenbdezi.

Pia Makinda aliwataka wanaandishi wa habari hapa nchini kuhakikisha kuwa wanakuwa wanatenda haki katika utendaji wao wa kazi na kuandika habari zenye tija na si kuandsika habari zinazoegamia upande mmoja.

Alisema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiandika habari za uchochezi ambazo hazina masdlahi na Taifa na badala yake zimekuwa sikisababisha malumbano.

Hata hivyo makinda alisema kuwa ofisi yake imedhamilia kuwaendeleza waandishi wahabri waliopo hapa nchini kielemu ili waweze kuwa na utaalam wa kutosha katika mambo mbalimbali na hasa kuandika habari za bunge ndio maana imeendeleza utaratibu wake wa kuwapewleka waanndishi katika nchi mbalimbali kuangalia na kujifunza mabunge mengine yanavyofanya kazi.

Aidha Makinda aliwataka wanawake kujiamini na hasa wanapopewa nafasi za uongozi na si kujidharau na kuona kama hawawezi kusimama mbele ya wanaume na kuongfoza kama ilivyo kwake anavyosimama mbele ya wabunge bila kujali kama ni mwanamke.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.