Habari za Punde

JUMADU. CHAWEDAMA WACHELEWESHA UVAAJI SARE MADEREVA


Na Amina Mohamed, MCC

MVUTANO kati ya jumuiya mbili zinazoshughulikia daladala JUMADU na CHAWEDAMA zimepelekea kusogeza mbele siku za uvaaji sare za madereva na makonda wa gari za abiria wa mjini.


Hapo awali kulikuwa na makubaliano kuwa madereva na makondakta walikuwa waanze kuvaa sare Agosti 1, mwaka huu kabla ya kutokea kwa mvutano huo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake mkuu wa mapato wa Baraza la Manispaa, Hidaya Masoud alisema mvutano uliotokea baina ya taasisi hizo umesababisha uvaaji sare kwa madereva na makondakta hao kuchelewa kuvaa sare.

Alisema Manipaa na Idara ya Usafiri na Leseni hazina pingamizi juu ya uamuzi wa madreva na makondakta kuvaa sare lakini kutokana na mvutano wajumuiya hizo kumesababisha tarehe za uvaaji sare kusogezwa mbele.

Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa jumuia hiyo zimekuwa zikivutana huku kila moja ikitaka usimamizi wa zoezi la kutoa sare kwa madereva na mkondakta.

Mkuu aleleza kuwa kati ya Jumuiya hizo mbili iliyosajiliwa katika Baraza la Manispaa ni CHAWEDAMA ambayo inasimamia uingiaji wa gari na kutoka katika vituo vya mjini.

Nae mwenyekiti wa jumuiya ya CHAWEDAMA, Muhammed Makame Njune, hakupinga suala la uvaaju wa sare kwa sababu ni amri iliotolewa na serikali ili kuleta maendeleo kwa jammii.

Mwekititi huyo alisema kuwa uvaaji wa sare kwa makonda na madereva ni jambo lenye umuhimu lakini kutokana na hali ngumu ya maisha wamependekeza kuwavisha sare katika maeneo wanayo yataka.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya JUMADU, Waziri Hashim Rajab hakupinga suala la ukataji wa sare huzo maeneo ya njee lakini kutokana na ubabaishaji wa rangi tofauti katika maduka ni bora zaidi kupitia katika jumuiya huyo ili kupatiwa taaluma kuhusu fomu hzo

Hata hivyo madereva wa gari mbali mbali za abiria wameiomba serikali ya pamoja na tasisi zinazo shughulika na uvaaji wa sare kupunguza gharama za umiliki wa sare hizo ili kila mmoja aweze kupata sare.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.