Habari za Punde

PEMBA WALALAMIKA KUPANDISHWA BEI ZA VIBALI

Na Habari Maelezo Pemba

Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wamesikitishwa na kitendo wanachodai kufanyiwa na Masheha wa Mkoa huo kwa kupandisha bei ya vibali vya kuuzia Mazao mbali mbali likiwemo zao la Karafuu kwa kutozwa shillingi elfu moja wakati Mkoa wa Kusinui Pemba hutoza shillingi mia tano tu.

Wamesema kiwango hicho wanachotozwa Wananchi wa Mkoa huo ni kikubwa mno nakinaweza kusababisha wananchi wa mkoa huo wenye Karafuu kidogo kuzirundika nyumbani hadi kuwa nyingi jambo ambalo Serikali halipendelei hata kidogo.


Wananchi hao wameyaeleza hayo leo wakati walipokutana na wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi yaFedha Biashara na Kilimo katika ziara yao walipokuwa wakivitembelea Vituo mbali mbali vya Ununuzi wa Karafuu vya Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC).

Wamesema kuwa bei inayotozwa na Masheha hao katika uuzaji wa vyeti vya Mazao sio sahihi ikilinganishwa na bei inayotolewa naWilaya ya Mkoani na Chake Chake ziopo Mkoa wa Kusini Pemba ambapo kila Wilaya hutoza Shillingi mia tano tu.

Wananchi hao wamesikitishwa sana kuona Fedha hizo zinazokusanywa na Masheha hao wamedai hazitumiki kwa lengo lililokusudiwa la kuzichangia Halmashauri za Wilaya mapato yake na badala yake wamedai kuwa huingia katika mikono ya watu wachache.

Masheha wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wamewaelezea wajumbe wa kamati hiyo iliopo chini ya Mwenyekiti wake Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin kuwa wao hununuwa vitabu hivyo vya Risiti kwa kila kimoja chenye kurasa mia mojkwa bei ya shillingi sitini elfu wakati wenzao wa Mkoa wa Kusini Pemba hunuwa kitabu kama hicho kwa shillingi elfu thalathin tu..

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Baraza la Wawakilishi Fedha, Biashara na Kilimo Salmini Awadh Salmin amewaagiza wakuu wa Wilaya ya Wete na Micheweni katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kulisimamia suala hilo nakulipatia ufumbuzi wa haraka iwezekavyo ili azma ya Serikali ya ununuzi wa Karafuu Katika Vituo vya ZSTC ifanyike bila ya matatizo yoyote yale

Amesema katika kipindi hichi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejikita katika uokoaji wa zao hilo la Karafuu hivyo malalamiko ya Wananchi yasiposhughulikiwa yanaweza kusababisha LENGO la Serikali lisifikiwe.
Afisa Mdhamini wa Wizara ya Biasahara Viwanda na Masoko Pemba Hemed Suleiman nae ameahidi kulichukuwa nakulifanyia kazi tatizo hilo ili lengo na azma ya Serikali yakulifufuwa zao hilo lifikiwe.

Hata hivyo Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi kwa ujumla imeridhishwa nakazi nzuri inayofanywa na ZSTC katika harakati za ununuzi wa zao hilo katika Vituo mbali mbali kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.