Habari za Punde

SHIRIKA LA HABARI ZANZIBAR LAANZA MATANGAZO YA REDIO SAA 24

Na Faki Mjaka-Maelezo ZANZIBAR

Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC)leo linatangaza rasmi matangazo yake ya saa 24 kwa upande wa radio tu.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Hasaan Abdallah Mitawi ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu.

Mitawi amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona kuwa umefika wakati wa kufanya hivyo ili kuwapa nafasi zaidi wananchi wa Zanzibar kupata matangazo mbalimbali kupitia shirika hilo kwa uande wa radio ambayo hupatikana sehemu kubwa ya Zanzibar kwa hivi sasa.

Amesema kuwa matangazo hayo ya saa 24 yatapatikna kwa kupitia mitambo yake ya FM ya Megahats 90.5 na 97.4 Unguja ambapo kwa upande wa Pemba yanapatikana kupitia 94.1 na 90.5

Mkurugenzi Mitawi ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuendelea kusikiliza matangazo mbalimbali kupitia shirika la utangazaji Zanzibar ili waweze kufaidika na matangazo yake.

Shirika la utangazaji Zanzibar lilikuwa likitangaza kwa muda wa masaa 18 kwa siku ambapo kuanzia leo litakuwa hewani masaa 24 kupitia mitambo yake hiyo ya FM.

Shirika la utangazaji Zanzibar ambalo lilianzishwa rasmi Februari 14 mwaka huu kabla ya hapo lilikuwa na idara za Televisheni Zanzibar na Sauti ya Tanzania Zanzibar ambapo Radio ya Sauti ya tanzania Zanzibar ilianziashwa rasmi machi 15, 1951 na ni Radio ya kwanza kuanzishwa Afrika mashariki.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.