Habari za Punde

CCM KUTOWATIMUA VIONGOZI WASTAAFU

Na Fatuma Kitima, Dar es Salaam

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa hakina mpango wa kuvunja katiba na wala kuondoa baadhi ya viongozi wastaafu katika kamati kuu kwasababu wanatambua umuhimu katika utendaji kazi wa watu hao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye alisema kuwa chama hicho hakiwezi kufikia mahali kuwaondoa viongozi hao kwa kuwa ni wanamaslahi katika kamati hiyo.


Nnauye alisema alishangazwa na chombo cha habari kimoja nchini kilichotoa habari kuhusu kung’olewa kwa viongozi katika kamati kuu kwa kuwa taarifa hiyo haikufanyiwa maamuzi na chama hicho.

Alisema pamoja na habari hiyo chombo hicho pia kimetoa tangazo ambalo halikutolewa na chama, hivyo wanaangalia taratibu na maadili katika taaluma hiyo kama kilichotumika ni sahihi.

“Viongozi hao bado wapo katika kamati kuu na haitafika wakati kuwaondoa”, alisema Nnauye.

Aidha alisema taarifa iliyotolewa na chombo hicho sio ya kweli hivyo amewataka viongozi na wananchi kuachana na habari hiyo ambayo inapotosha jamii.

Nnauye alisema kuwa taarifa hizo za propaganda labda zimetengezwa kwa maslahi yao wenyewe, au ya mtu binafsi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.