Na Khamisuu Abdallah
WANUNUZI wa Biashara katika soko la Mwanakwerekwe wamelalamikia suala la uchafuzi wa mazingira sokoni hapo hususan wakati wa kipindi cha mvua.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi Mwanakwerekwe wananchi ambao mara kwa mara wanakwenda kwenye soko hilo walisema hali ya Mazingira hairidhishi katika soko hilo kutokana na utupaji taka ovyo.
Aidha, walisema kuwa wananchi wanaotumia soko hilo wawe na tabia ya kusafisha kila mara kwani wakiendelea kutupa taka ovyo kunapelekea kuharibika kwa haiba ya kisiwa cha Zanzibar.
Nae Msaidizi wa Soko hilo Said Omar, Talib alisema ni kweli hali ya uchafu katika soko hilo ipo lakini kwa asubuhi katika mkusanyiko wa watu katika soko hilo na idadi kubwa ya wafanyabiashara na kutojali
namana ya kila mmoja kudhibiti sehemu alionayo kwa hali ya usafi katika soko hilo.
''Nikweli hali ya uchafu wa soko hili upo lakini kwa nyakati za asubuhi sababu wakati huo kunakuwa na wanunuzi wengi na wauzaji hivyo kunakuwa hakusafishwi hadi pale saa sita ndio watu wa Manispaa
wanakuja kufanya usafi,''aliserma.
Hata hivyo, alifahamisha kwamba wafanyabiashara ni vyema kujua wajibu wao katika soko hilo kwa lengo la kufanya biashara kwa kuweka vitu vizuri.
Hivyo amewataka wafanya biashara wote kuhakikisha bidhaa zao wanazipanga vizuri sokoni hapo na kuweka maeneo safi ili kujiepushia usumbufu na kuweza kupatikana kwa maendeleo sokoni hapo.
No comments:
Post a Comment