Habari za Punde

BENKI YA KCB YAMWAGA MISAADA YA MADESKI SKULI YA MWERA MSINGI ZENJ.






 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa shukrani zake kwa Uongozi wa Benki ya Biashara ya Kenya KCB, kwa msaada wao kusaidia shughuli za jamii, katika sherehe za kukabidhi Madeski 168 kwa Skuli ya Mwera Msingi.   
Meneja Masoko Abdull Mshangama, akitowa maelezo mafupi ya msada huo wa madawati kwa skuli ya Mwera katika sherehe za makabidhiano yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya Mwera.    
 Meneja Huduma wa Benki ya Biashara ya KCB Francis S. Mandala, ambaye amesoma katika skuli hiyo, akitowa maelezo ya shughuli za Benki hiyo inazofanya na kujali shughuli za Jamii.  
Baadhi ya Madeski yaliotolewa na Benki ya Biashara ya KCB,kwa ajili ya Wanafunzi wa Skuli ya Mwera Msingi yakiwa katika viwanja vya skuli hiyo baada ya kukabidhiwa. 

3 comments:

  1. Ni jambo la kushukuriwa kwa yule alonacho kumsaidia asonacho au anaehitaji lakini wakati mwengine pia inahitaji au iko haja ya kutowa kilicho kizuri ambacho wewe mtoaji unakipenda.
    Nadhani Madeski ya mbao yameshapitwa na wakati sana sana kwani hata computer haitoweza kukaa hapo na pia hayaleti sura nzuri.Nahisi iko haja ya wanafunzi kujengewa mazingira yao mazuri ili wapate ule moyo wa juhudi.
    Jambo jengine ni kutokana na jinsi nionavyo hao wafanya kazi wa Bank yenyewe wako ovyo ovyo,iweje watu wa ngazi ya juu katika Bank kuvaa fulana za msewe na iwapo ndio sare zao hapo wamefeli na kwa muono wangu siwezi kuzipeleka pesa zangu kwao.

    ReplyDelete
  2. mchangiaji namba moja! kwani kama huna cha kuchangia lazima uchangie utumbo uliokuwa hauna mbele wala nyuma!

    ReplyDelete
  3. Hongera mchangiaji wa kwanza kwa kutoa mtazamo wako!
    Ama mimi nna mawazo tofauti na hayo.

    Huhusu benki ya KCB, kwakweli inapaswa kupongezwa kwa juhudi zao za kuisaidia serikali kuboresha elimu. KCB wanafanya kile ambacho PBZ walishindwa kwa takriban miaka 48 wakiwa benki kubwa pekee ya biashara z'bar.

    Kuhusu suala la 'quality' mimi nadhani inategemea uwezo, mazingira na hadhi ya kiuchumi ya eneo husika na kwa mazingira yetu na hata msaada wa stuli au mabusati basi unafaa kulingana na mazingira yetu. Labda mwenzetu hujapata fursa ya kutembelea skuli mbali mbali hapa z'bar hususan mashamba kama vile Kilindi Pemba, Kiongwe na michamvi Unguja n.k.

    Ama suala la kuvaa fulana za 'msewe' mnake za msewe hua nyeupe, nadhani ni kwa sababu ya shughuli iliyo mbele yao pamoja na dhamira ya kujitangaza zaidi. Kwamba hutapeleka fedha zako huko, si shangai hii ni changamoto kwa waz'bari wengi, tumekua wazito kutumia huduma za kibenki
    Mwanzoni tulijidai tunaogopa riba, sasa hivi tuna akaunti za shari pia hakuna anaefungua. Nimpaka tulazimishwe makazini au tukitaka kujiunga na vyo..kazi kweli kweli!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.