Na Faki Mjaka - Maelezo
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Balozi amesema Israel
itatuma timu ya Wataalamu kuja kufanya utafiti wa Ugonjwa wa Moyo ambao umekuwa
ukiwashambulia watoto hasa kutoka maeneo ya Pemba na kutafuta njia nzuri za
kuweza kukabiliana na tatizo hilo .
Balozi Idd
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuwasili uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Abeid Aman Karume kutoka ziara yake
ambapo alizitembelea Nchi za Israel ,
Cuba
na Ras El kheima.
Amesema kuwa Israel imepata mshangao mkubwa kwa kuona kuwa
watoto wadogo wengi kutoka Zanzibar wanakabiliwa
na matatizo hayo ya ugonjwa wa moyo jambo ambalo si la kawaida kwa hivyo
wameona iko haja ya kuja Zanzibar
kufanya utafiti juu ya maradhi hayo.
Balozi Seif
amesema kuwa mbali ya maradhi hayo Israel
imeahidi kutoa nafasi za mafunzo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwani wao
wanachuo maalum cha kufundishia suala hilo
kutokana na nchi yao
kuwa ni jangwa kwa hivyo wanautaalamu wa kutosha.
Akizungumzia juu
ya sula la kilimo cha ufugaji wa Samaki amesema kuwa Isarael pia ipo tayari
kusaidia Zanzibar kwa wananchi walioanzisha
ufugaji wa Samaki na zaidi kisiwani Pemba ili
waweze kufanya shughuli hiyo kwa utaalamu zaidi na kujipatia kipato zaidi.
Kuhusu suala la
maafa Balozi Seif amesema kuwa Israel
ipo tayari kuisadia Zanzibar kwa kuipatia vifaa
na mbinu za kuweza kujikinga na maafa na pia kuwasomesha wananchi wa Zanzibar kuhusu masuala hayo na tayari nafasi mbili kwa
watu wa Zanzibar
wamepatiwa kwenda nchi hiyo mwezi ujao
Kwa upande wa Cuba
Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa nchi hiyo imekubali kuongeza madaktari Zanzibar wa maradhi mbalimbali na pia kutoa madaktari
watakaoweza kuwafundisha wanafunzi wanaosomea fani hiyo hapa Zanzibar .
Aidha Balozi Seif
amesema mbali na kuleta madaktari pia patakuwa na nafasi kwa nchi hizo mbili
kubadilishana uzoefu katika fani hiyo kwa kutembeleana.
Mbali na shuguli
hizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alifanyiwa matibabu ya Macho nchini humo ambapo hali yake ipo nzuri na
yakuridhisha.
Huko Ras El Kheima
alisema kuwa nchi hiyo imeendelea katika ufugaji wa Lulu ambapo Zanzibar inaweza kufaidika katika soko hilo
kwa wataalamu kutoka nchi hiyo kuja Zanzibar
kuweza kuwafundisha wananchi ili na wao waweze kutoa zao hilo kwa wingi na soko kuu kuwa huko.
Makamo wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd aliondoka Zanzibar May 5,2012 kwa kuanzia
ziara yake nchini Israel,Cuba na hatimaye Ras El Khaeima na kurejea Zanzibar
June 2,2012.
No comments:
Post a Comment