Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SIKU chache baada ya timu ya taifa ya soka la wanawake Twiga Stars kuchapwa na Ethiopia katika kusaka fainali za mataifa ya Afrika, Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa, amejiuzulu.
Twiga Stars iliambulia kipigo cha bao 1-0 mikononi mwa Ethiopia na kuondolewa katika michuano ya Afrika kwa soka la wanawake katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kufutia awali kufungwa 2-1 jijini Adis Ababa.
Kocha huyo aliyekuwa ameanza kupata mafanikio taratibu akiifundisha Twiga Stars, alishutumiwa na mashabiki kuwa ndio chanzo cha timu hiyo kupoteza mchezo huo na kutolewa katika ngarambe hizo ambazo pia hutoa wawakilishi wa Afrika katika Kombe la Dunia kwa soka la wanawake.
Kutokana na lawama hizo, Mkwasa juzi usiku Mkwasa alikaririwa na blogu ya Bin Zubeiry akitangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa kocha mwengine kuchukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho.
Aidha, kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars, amesema ameamua kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya na pia timu hiyo kutothaminiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mara kadhaa, wachezaji wa Twiga Stars wamekaririwa wakilalamikia ukata na kukosekana kwa ligi ya maana ya soka la wanawake mbali na ile ya mkaa wa kisoka wa Kinondoni, ambayo nayo imepoteza ladha.
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Jumamosi, Mkwasa alisikika akizungumza baada ya mchezo wa Jumamosi akisema uwezo wa Twiga Stars umefikia kikomo.
Mkwasa pia alisema timu hiyo haikuwa na maandalizi mazuri na TFF haikuonekana kuijali kabisa.
Hata hivyo, kauli hiyo imeibua wasiwasi kwa wadau na mashabiki wa spoa ncbini wakidai kuwa si uwezo wa wachezaji uliofikia kikomo, bali ni wa mwalimu aliyekosa mbinu za kisasa kuwafundisha. .
Mkwasa amesema pamoja na kuona uwezo wa wachezaji wake umefikia kikomo, lakini hawapaswi kulaumiwa kwani walicheza kadiri ya uwezo wao.
No comments:
Post a Comment